Mradi wa Kinyerezi 1 kukamilika mwezi Juni; Wafikia asilimia 80 ya ukamilishwaji wake; Watumia Dola Milioni 167. 2 hadi sasa

      

KA1Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wanja Mtawazo ( kulia) akisalimiana na Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi ( kushoto) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo la mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I. Kamati hiyo inafanya ziara katika miradi ya umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini ya tanzanite katika mkoa wa Manyara ili kujionea maendeleo ya sekta hizo.
KA2Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (kulia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mradi Mkazi wa Kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway inayojenga mtambo wa Kinyerezi I Markkli Repo ( wa pili kutoka kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo la mtambo huo ili aweze kuwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye ziara katika mitambo hiyo.
KA3Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima (kulia) akielezea maendeleo ya ujezi wa mtambo wa Kinyerezi I mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (wa tano kutoka kulia), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
KA4Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi (katikati) akisisitiza jambo katika ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga na kulia ni Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima
KA5Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Felchesmi Mramba akielezea mikakati ya shirika la Tanesco kuboresha huduma za umeme nchini kote.
……………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima amesema kuwa mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu.
Mhandisi Jilima aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika mtambo huo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara ya kutembelea miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini aina ya tanzanite katika mkoa wa Manyara.
Mhandisi Jilima alisema kwa sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 na kufafanua kazi inayofanyika kwa sasa ni kumalizia utandazaji wa nyaya, ufungaji wa mabomba ya maji na gesi pamoja na ujenzi wa barabara za ndani.
Alisema kuwa ofisi kwa ajili ya watumishi pamoja na karakana kwa ajili ya kuhifadhia mitambo imekamilika.
Akielezea gharama za mradi huo Mhandisi Jilima alisema mpaka sasa serikali imelipa kiasi cha Dola za Marekani milioni 167.2 na kuongeza kuwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 15 kinatarajiwa kumaliziwa kabla ya kukamilika kwa mradi.
Akielezea changamoto katika utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Jilima alieleza kuwa awali changamoto kubwa ilikuwa ni ukamilishwaji wa mradi wa bomba la gesi ili waweze kutumia gesi hiyo katika kuzalisha umeme lakini kutokana na kasi ya mradi huo kuwa ya kuridhisha wana imani kuwa gesi itaanza kuzalishwa mapema kabla ya kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi 1
“ Ndugu wajumbe, awali tulikuwa na wasiwasi wa kupatikana kwa gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kupitia mradi wa Kinyerezi 1 kutokana na mradi wa bomba la gesi kuwa na changamoto nyingi, lakini baada ya kuona mradi wa bomba la gesi uko katika hatua nzuri yaani zaidi ya asilimia 90, tunaamini kuwa mara mtambo utapokamilika, gesi itakuwa imekwishaanza kuzalishwa na hapo ndipo tutaanza kuzalisha umeme mara moja,” alieleza Mhandisi Jilima
Akielezea fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi huo, Mhandisi Jilima alieleza kuwa mradi wa Kinyerezi I ulikwishafanya tahmini pamoja na kulipa fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mtambo huo tangu mwaka juzi.
Wakati huohuo wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walipongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mtambo huo na kuitaka serikali kukamilisha malipo ya kiasi kilichobaki cha Dola za Marekani milioni 15 ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*