Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, ametoboa siri sababu za Rais Jakaya Kikwete
kumhamisha Dk. Harrison Mwakyembe (pichani) katika Wizara ya Uchukuzi
kwenda Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Akizungumza juzi na
mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kyela,
alisema Rais Kikwete alimhamisha Dk. Mwakyembe katika Wizara ya Uchukuzi
kwa sababu anaifahamu vyema Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
kwa kuwa alishawahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Masharika na pia
mwanasheria.“Dk. Mwakyembe amehamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kutokana na kuwa anaielewa vizuri na pia ni mwanasheria
aliyebobea hivyo Rais Kikwete aliona atakuwa msaada mkubwa katika
kuisaidia nchi,” alisema.
Hatua ya
Waziri Mkuu Pinda kutoa ufafanuzi huo kulifuatia kuwapo kwa malalamiko
kutoka kwa baadhi ya wananchi walihoji kwanini Dk. Mwakyembe amehamishwa
Wizara ya Uchukuzi ambayo aliimudu vyema kwa kudhibiti vitendo vya wizi
hususani katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na upitishwaji wa
dawa za kulevya katika viwanja vya ndege.
Mwishoni
mwa mwezi uliopita, wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
walifanya mkutano Jijini Nairobi na Rais Kikwete alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa EAC huku Waziri Mwakyembe akichaguliwa
Comments