RAIS MUGABE AWASIRI ARUSHA NA UTITITRI WA WALINZI, AIPONGEZA TANZANIA NA HAYATI NYERERE

 Rais Robert Mugabe (katikati) wa Zimbabwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, akishuka kwa uangalifu kwenye ngazi huku akiwa amezingirwa na walinzi wake alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, tayari kufungua Kongamano la Viongozi wa Vijana wa Afrika na China lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UV/CCM) jijini Arusha. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Rais Robert Mugabe (katikati) wa Zimbabwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), akipewa zawadi ya shada la maua na mtoto Khairat Said, alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, tayari kufungua Kongamano la Viongozi wa Vijana wa Afrika na China lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UV/CCM) jijini Arusha. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Komredi Mugabe ameisifu Tanzania na Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere kwa kazi kubwa aliyofanya kwa kuhakikisha nchi nyingi za Afrika na hasa kusini mwa Afrika zina pata uhuru.
 Komredi Mugabe akipita katika ya gwaride ililoandaliwa wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa KIA
 Komredi Mugabe (kulia) akiambiwa jambo na Komredi Kinana alipokuwa akiangalia ngoma ya utamaduni
 Ngoma ya utamaduni ya jamii ya kimasai ikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Komredi Mugabe wa Zimbabwe.
 Komredi Robert Mugabe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto). Kulia ni Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
 Rais Robert Mugabe (katikati) wa Zimbabwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akiangalia ngoma za utamaduni alipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, tayari kufungua Kongamano la Viongozi wa Vijana wa Afrika na China lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UV/CCM) jijini Arusha. 9PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele akizungumza na wanahabari baada ya kumlaki Rais wa Zimbabwe, Komredi Mugabe kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo. Mugabe alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika jijini Arusha .
 Rais Jakaya Kikwete akipatiwa tuzo ya juu ya heshima ya kutambua mchango wake katika kuhamasisha amani na utulivu Afrrika. Tuzo hiyo anakabidhiwa na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika, Francine  Furaha Muyumba katika kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM.
 Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika Kongamano hilo kwenye Hoteli ya Ngurdoto, jijini Arusha.
 Baadhi ya vijana wakipiga picha za kumbukumbu wakati Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika kongamano hilo.
 Rais Jakaya Kikwete  akiondoka huku akisindikizwa na Komredi Kinana baada ya kuhutubia mkutano huo.
 Kinana akizungumza jambo na Rais  Jakaya Kikwete  alipokuwa akimsindikiza baada ya kuhutubia mkutano. Kushoto ni  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
 Bendera za nchi mbalimbali ambazo wajumbe wake wanashiriki katika kongamano hilo zikipepea nje ya ukumbi klwa mkutano katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha
 Komredi Kinana akizungumza na mmoja wa wajumbe wa kongamano hilo
 Walinzi wa Rais Mugsbe wa Zimbabwe wakiimarisha ulinzi wakati kiongozi huo akiremka kutoka kwenye gari
 Komredi Mugabe (katikati) akipanda ngazi kwa uangalifu kuingia kwenye ukumbi wa mkutano
 Komredi Mugabe akiingia ukumbini huku akisindikizwa na Komredi Kinana
 Komredi Mugabe akionesha ushupavu alipokuwa jukwaa kuu tayari kufungua kongamano hilo
 Komredi Mugabe akiwa na Komredi Kinana pamoja na Wasira meza kuu kabla kufungua kongamano hilo
 Komredi Kinana akihutubia katika Kongamano hilo kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha
 Katibu Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Zhou Chang Kui akizungumza katika kongamano hilo
 Mwenyekiti wa AU, Robert Mugabe akihutubia katika Kongamano hilo la Vijana Afrika
Sehemu ya wajumbe wa kongamano hilo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA