Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya
Iringa likiwa limeteketea kwa moto jana ,picha nyingine wazazi na
wanafunzi wakiwa nje ya Bweni hilo ,na picha nyingine na mmoja
kati ya majeruhi katika tukio hilo la Moto akiwa katika kituo cha
afya Idodi (picha na Francis Godwin Blog)
Mmoja wa wanafunzi akiokolewa
Mmoja wa wanafunzi akiokolewa
Na Francis Godwin,Iringa
UKIWA
umepita mwezi mmoja toka sehemu ya bweni la wasichana katika
shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa kuteketea
kwa moto ambao chanzo chake kilitajwa kuwa ni hitirafu ya umeme ,
moto mwingine tena umeibuka na kuteketeza sehemu ya bweni hilo
iliyobaki huku wanafunzi zaidi ya 14 wakijeruhiwa .
Wakielezea
juu ya tukio hilo wanafunzi wa shule hiyo walisema kuwa moto
huo ulianza kuteketeza bweni hilo juzi (jumapili) majira ya saa 9
Alhasiri wakati wanafunzi wote wakiwa madarasani wakiendelea
kujisomea.
Alisema mmoja
kati ya wanafunzi kuwa wakiwa katika mdahalo wa wanafunzi shuleni
hao walisikia kelele kutoka nje ya darasa juu ya kuwaka kwa
bweni hilo ila hawakuweza kutilia manani sana wakijua ni utani ila
kulingana na kelele zilivyozidi ndipo walilazimika kutoka kwenda
eneo la bweni hilo la Benjamini Mkapa ambalo hutumiwa na wasichana
na kukuta moto ukiwa umeshika kasi zaidi na hivyo kuanza kuuzima
moto huo kwa kushirikiana na walimu na baadhi ya wananchi
waliofika kwa wakati eneo hilo.
Hata
hivyo wanafunzi hao ambao hawakutaja kutajwa majina yao
kiusalama walisema kuwa chanazo cha moto huo inaonyesha ni
hitrafu ya umeme inayosababishwa na baadhi ya wanafunzi wenzao ambao
si waaminifu wenye tabia ya kuchaji simu zao bwenini kwa
kuchubua nyaya za umeme .
Kwani
walisema kuwa mabweni hayo hayana sehemu maalum za kuchajia simu
huku asilimia kubwa ya wanafunzi wanatumia simu hivyo kutokana na
kuhofia kukamatwa na simu wamekuwa wakitumia muda wa kwenda
madarasani kwa ajili ya kuchaji simu zao kwa siri kubwa .
MKuu
wa shule hiyo Bw Christopher Mwasomola alisema kuwa kwa
kawaida wanafunzi wa shule hiyo hawaruhusiwi kuwa na simu japo
siku za jumamosi na jumapili uongozi wa shule hiyo huwa
unawapa simu wanafunzi kwa ajili ya kuwasiliana na jamaa zao.
"Kusema
chanzo cha moto huu ni simu bado siungi mkono kwani hakuna
sehemu ya kuchajia simu katika mabweni ya wanafunzi hivyo bado
tunaendelea na uchunguzi zaidi ili kujua chanzo hasa cha moto huu
"
Alisema kuwa katika
tukio la moto lililotokea mwezi uliopita jumla ya madogoro 190
yaliteketea kwa moto na katika tukio hilo la pili jumla ya
madogoro 48 ambayo ni mali ya wanafunzi pamoja na mashuka yameteketea
kwa moto na vitu mbali mbali vya wanafunzi hao huku hasara
nyingine iliyojitokeza ikiwemo ya jengo hilo .
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Bi Angelina Mabula
akizungumza na wananchi wa Idodi na walimu wa shule hiyo
alitaka kufanyike kwa uchunguzi wa kina ila kuweza kujua chanzo
cha matukio hayo mfululizo katika shule hiyo ikiwa ni pamoja na
kuchunguza umiliki wa ardhi hiyo ambayo shule hiyo imejengwa kama
wapo wenye dukuduku basi kukaa nao ili kuondoa tofauti zilizopo.
Wakati
huo huo mkuu huyo wa wilaya ameagiza shule hiyo kufungwa kwa
muda wa wiki mbili ili kufanya uboreshaji wa bweni hilo ambalo
limeteketea lote kwa moto na kuwaomba wananchi kujitolea nguvu
zao ili kuharakisha ukarabati wa jengo hilo.
Mbunge
wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi mbali ya kuwapa pore walimu na
wanafunzi wa shule hiyo kwa tukio hilo bado alisema kuwa amepokea
kwa masikitiko makubwa tukio hilo na kwa sasa ataungana na
wananchi wa Idodi katika uboreshaji wa jengo hilo ili wanafunzi
waweze kurejea kwa wakati .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Bw Lukuvi alisema
anachokifanya kwa sasa ni kutafuta wahisani mbali mbali ili
kufanikisha ukarabati wa jengo hilo kwa kushirikiana na wananchi
wake .
MWISHO
Comments