Vijiji viwili kupata maji mwishoni mwa wiki hii

           

2
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Serengeti Marwa Mulaza(kushoto aliyesimama), akisoma taarifa ya mradi wa Maji wa kijiji cha Nyagasense mbele ya Mgeni Rasmi Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe.
3
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyagasense baada ya kuweka jiwe la Msingi na kutembelea mradi wa maji wa kijiji hicho.
4
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyagasense wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani).
5
Mkazi wa kijiji cha Nyagasense Christina Machota akiuliza swali kwa Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe.
6
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiwa ameambatana na wenyeji wake wakielekea kukagua chanzo cha mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
7
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akikagua bwawa la maji ya Mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
8
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi kuzindua Mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
9
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (katikati), akikagua miundombinu ya mradi wa maji wa Rung’abure.
……………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO, Musoma
WAKAZI wa vijiji viwili vya Nyagasense na Rung’abure vilivyoko kwenye wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamehakikishiwa kuanza kupata maji ifikapo mwishoni mwa wiki hii kufuatia wakandarasi wanaojenga miradi ya maji ya vijiji hivyo kuahidi kufikisha maji katika kipindi hicho.
Akitoa ahadi kwa Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Nyagasense, Mhandisi wa mradi wa maji wa kijiji hicho John Mapande amesema maji yataanza kutoka siku tatu kuanzia leo.
Mhandisi Mapande alitoa ahadi hiyo wakati Waziri Prof. Maghembe akizungumzia matumaini ya kukamilika kwa mradi huo wa maji ambapo aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kukaa mkao wa kunywa maji.
“Ninawomba sana mkae mkao wa kunywa maji kwa sababu nimeona kwa macho yangu na nimeridhika, vinginevyo nisingeweka jiwe la msingi, hivyo katika kipindi kifupi maji yatafika huku mitaani” alisema Waziri Prof. Maghembe
Baada ya kutoa matumaini hayo, Waziri Prof. Maghembe alimuita mkandarasi wa mradi huo na kumsihi kukamilisha mradi huo na kwamba fedha zake zilizobaki atalipwa, na mazungumzo yao yailikuwa hivi:
Waziri: Mkandarasi uko wapi?
Mkandarasi: Niko hapa mheshimiwa Waziri.
Waziri: Sasa wewe ukamilishe mradi wangu, ile miezi sita ikiisha fedha zako zitakazokuwa zimebaki tutakulipa, kwa hiyo we maliza mradi haraka wiki ijayo mimi ninywe maji hapa kabla sijakwenda Dar es Salaam.
Mkandarasi: Nitajitahidi Mhe Waziri kukamilisha.
Waziri: Jitahidi, maana kazi iliyobaki ni kidogo sana kukamilisha huu mradi
Mkandarasi: Ni kazi ya siku mbili au siku tatu maji yatakuwa yameshatoka
Waziri: Eeh sasa kazi ya siku mbili tatu mimi nitakuwa Mara hapa, nataka nikienda Mugumu nisimame hapa ninywe maji.
Kwa upande wa mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure, Waziri Prof. Maghembe alimuagiza mkandar akafunge jenereta na kupeleka pampu na kuifunga ili maji yaanze kusukumwa kuanzia leo.
Waziri Prof. Maghembe alichukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wananchi kuzuia malori yanayopeleka jenereta na pampu kwenye eneo la mradi, kupita kwenye eneo lao, lakini Serikali ya kijiji ilimuhakikishia Waziri kwamba wananchi hao wameruhusu gari ipite.
Waziri: bwana mkadarasi yuko wapi
Mkandarasi: Nipo hapa mheshimiwa
Waziri: Nimemuagiza huyu mkandarasi kesho alete jenereta ifungwe kwenye nyumba ya genereta na alete pampu pale ifungwe ili maji yaanze kusukumwa kesho (leo).
Kwa hiyo muangalie atafunga kesho labda jioni atakuwa amekamilisha, lakini hata kama hakukamilisha Alhamisi atakamilisha, Alihamisi akikamilishwa bado nitakuwa mkao wa Mara.
Kwa hiyo siku ya Alhamisi kwa uhakikka wataanza kusukuma maji, nimeona kazi nyingi hazijakamilika, lakini hiyo ikamilishwe kesho na Alhamisi ili sasa wakati wanaendelea na kazi nyingine mnaendelea kunywa maji.
Baada ya kuzungumza hayo, wananchi walipiga vigelegele na makofi kuonesha kufurahishwa na hatua hiyo.
Wakizungumza kufurahishwa na matumaini hayo ya kupata maji, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyagasense wamesema wamefurahi kupata ujio wa Waziri na hatimaye kuahidiwa kupata maji.
“Kwa kweli tumefurahi sana kupata ujio wa Waziri wa Maji na tumeridhika na ahadi ya kupata maji wiki hii kwa sababu tumekosa maji kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunapata shida ya kuyapata” alisema mkazi wa kijiji hicho Christina Machota.
Mradi wa Maji wa kijiji cha Nyagasense unaotekelezwa chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira, unatumia chanzo cha kisima kirefu chenye uwezo wa kutoa maji lita 6000 kwa saa na utakapo kamilika utahudmia watu 5,530 na mifugo 2620.
Mradi huo una jumla ya kilometa 19.54 za mtandao wa mabomba ya maji na vituo 20 vya kuchote maji na birika 2 za kunyweshea mifugo.
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Rung’abure, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Serengeti Marwa Mulaza, alisema una chanzo cha maji mtiririko na hutoa lita 10,000 kwa saa na ulianza kutekelezwa Oktoba mwaka2013.
Alisema mradi huo utakapokamilika utahudumia watu 3, 457 na mifugo na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Aprili mwaka huu 2015.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.