WATU SABA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KUTEKA NA KUKATA KIGANJA CHA MTOTO ALBINO SUMBAWANGA

Jeshi la polisi mkoani rukwa linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha kikatili cha kukata kiganja cha mkono wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka sita, katika kitongoji cha kikonde kata ya kipeta wilaya ya sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo wamemjeruhi mtoto huyo mkono wa kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa rukwa kamishna msaidizi wa polisi Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo kwenye kitongoji hicho cha kikonde, ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu wa kilimo na kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine watatu wenye ulemavu wa ngozi. 
ACP.Rwegasira pia amesema kwenye msako huo mkali, wamefanikiwa kuwakamata watu wanane wanaojihusisha na uganga wa jadi na upigaji wa ramli chonganishi, ambacho ni chanzo kikubwa cha kusababisha vifo na kujeruhiwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina. 

Mtoto baraka na mama yake mzazi wamelazwa kwene hospitali ya rufaa ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha waliyoyapata wakati wa purukushani za kumshambuliwa mtoto huyo.

No comments:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.