ZIARA YA KINANA YALINYAMAZISHA JIJI LA ARUSHA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Wafanyabiashara alipotembelea Soko la Kilombero, jijini Arusha ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alifanikisha kuushawishi uongozi wa halmashauri ya jiji hilo kukutana na uongozi wa soko hilo, kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara wa soko hilo

Kinana ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Arusha Mjini, aliwastajabisha wakazi wa jiji hilo alipoamua kutembea kwa miguu. Licha ya jiji hilo kuzoeleka kwa vurugu za kisiasa, jana lilikuwa shwari kabisa.
Komredi Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano katika soko hilo.

Komredi Kinana akishiriki upondaji wa kokoto alipotembelea kikundi cha Wajasiriamali cha wachimba mawe na waponda kokoto cha Elerai, jijini Arusha.
Mama ambaye ni mwanachama wa kikundi hicho akiendelea na kazi ya kuponda kokoto.
Mwananmke ambaye ni mwanachama wa kikundi hicho akilalamika mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Chrisopher Kangoye kwamba ameporwa eneo hilo linalotumiwa na kikundi hicho hivyo anataka haki itendeke ili arudishiwe.
Komredi Kinana akizindua tawi la CCM la Olmot.
Akina mama wakishangilia baada ya Komredi Kinana kuzindua Tawi la CCM LAOlmot jijini Arusha.

Kinana akishiriki uchimbaji wa mtaro katika mradi wa maji wa Olmot jijini Arusha.
Komredi Kinana akishiriki kuchimba mtaro alipokagua ujenzi wa Barabara ya Sombetini-Kwa Mrombo jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana akiwa na wanachama wa Chama cha Wasanii wa uhigizaji wa filamu Arusha, Komredi Kinana baada ya kuzindua raasmi ofisi yao jijini Arusha
Komredi Kinana akizungmza baada ya kuzindua tawi laCCM la Oysterbay, eneo la Unga Limited
Katibu Mkuu wa CCM, Komnga Ltd kwenda Soko la Kilombero jijini Arusha

Komredi Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM wakipata mlo kwa Mama Lishe katika Soko la Kilombero jijini Arusha
Muuza matunda akisalimiana na Komredi Kinana

Mama Lishe wakishangilia baada ya kumuona Komredi Kinana sokoni hapo
Mwendesha bodaboda akiwasha pikipiki iliyozinduliwa na Komredi Kinana aktika Kata ya Lemara kwa ajili ya kikundi cha waendesha boda. Bodaboda hiyo imetolewa na Diwani wa Kata hiyo. Kinana ameahidi kuwaandalia utaratibu wa kukopa pikipiki a wanachama 35 wa kikundi hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA