ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC KATIKA MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA


1
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo.
Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
New Picture (2)
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za gharama nafuu eneo la Unyankindi Singida na kukuta mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizoakiwa amejenga ukuta usilingana na viwango vilivyowekwa na NHC katika miliki zake inazojenga.
New Picture (4)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na mfanyakazi aliyestaafu utumishi wake NHC Dr. Allan Kabogo (wa pili kutoka kulia) walipomkuta eneo la Misigiri Wilaya ya Iramba akiwa anajishughulisha na biashara na huduma za kitabibu. Ujumbe huo ulifurahishwa kuona mstaafu wa NHC anaishi maisha ya furaha na matumaini makubwa.
New Picture (5)
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.
New Picture (6)
Nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga zikiwa katika hatua ya linta tayari kukamilishwa na kuuzwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo mengine watakaohitaji.
New Picture (7)
Utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama za nafuu unaotekelezwa na NHC katika mikoa 23 hivi sasa unatoa ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi hiyo kama wananchi hawa walivyonaswa na kamera ya NHC Wilayani Igunga jana.
New Picture (8)
Meneja wa NHC Mkoani Tabora Bw. Erasto Chilambo akiwatembeza viongozi wa Shirika waliotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani Igunga kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (9)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa kisima cha maji kinachotumiwa na vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.
New Picture (10)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiangalia namna mchanga wa kufyatulia matofali yanayofungamana unavyoandaliwa alipotembelea vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega jana. Vikundi hivi vilipewa mashine ya kufyatulia matofali na NHC kama sehemu ya kusaidia vijana ajira nchini.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa mchango wa kununua sementi kwa vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.Vikundi hivyo sasa vinapata kazi za kuwatengenezea wateja mbalimbali matofali hayo na hivyo kuwa na ajira endelevu.
New Picture (12)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakionyesha na Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo ramani yaeneo lililopewa NHC ili kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Nzega.
New Picture (13)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Bw. Mwikuka juu ya hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
New Picture (14)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akisalimiana na mafundi ujenzi alipotembelea mradi wa nyumba 50 za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
New Picture (15)
Mkurugenzi wa Usimamaizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akishiriki ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama mara baada ya Uongozi wa Shirika kutembelea mradi huo jana.
New Picture (16)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na NHC ili kuwawezesha wananchi wengi kumudu bei ya nyumba hizo alipotembelea nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ili kuukagua mradi huo jana.
New Picture (17)
Mkurugenzi wa redio Kahama FM Bw. Marco Mipawa akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alipotembelea studio hizo ili kufafanua namna wananchi wanavyoweza kununua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama jana. Ujenzi wa nyumba hizo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kuuzwa kwa wananchi.
New Picture (18)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoa wa Shinyanga(hawapo pichani) akisisitiza watende kazi zao kwa mtizamo wa kibiashara na kuongeza tija na kwamba hatasita kumuondoa kazini mtumishi yeyote wa Shirika ambaye atashindwa kufikia malengo aliyopewa.
New Picture
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akibatilisha eneo la kujenga nyumba ya biashara mjini Singida kwa Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya B.H Ladwa inayojenga jengo hilo. Kwa sasa jengo hilo litajengwa mbele ya jengo la Singida Motel ili kuweza kuvutia wafanyabiashara watakaopanga katika jengo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA