ZIARA YA WAZIRI MKUU TOKYO JAPAN

      

4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo  kutoka kwa Mbunge na Naibu Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Bw.Shigeki Iwai kuhusu kipeperushi chenye picha zinazoonyesha kilimo cha  chai kuzunguka mlima Fuji nchini Japan katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo  Machi 16, 2015.
(Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
1
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya vyakula vya  Kitanzania vilivyosindikwa  kitalaamu, Afisa Mtendaji Mkuu  na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Kampuni ya Sumitomo ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015.  Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Masuala ya Miundombinu ya Umeme wa kampuni hiyo, Tsutomu Ben Akimoto.
2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiagana  na  Afisa Mtendaji Mkuu  na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Kampuni ya Sumitomo Corporation  Corporation ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae (wapili kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015.  Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyrezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza kuda wake, Salome Sijaona, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Batilda Burian.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipata Maelezo  kutoka kwa Ofisa wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Noriko Tanaka kuhusu Treni inayofanyakazi bila dereva katika jiji la Tokyo wakatia lipotembelea Ofisi za Kampuni inayoendesha treni za aina hiyo ili kujifunza namna ya kusafirisha abiria kwa njia  ya reli katika majiji Machi 16, 2015.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI