ZIARAYA WAZIRI LUKUVI MWANZA

      

1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Bunge wa mambo mbalimbali yanayotarajiwa kufanywa na Wizara yake ili kuongeza ufanisi ikiwa ni pamoja na kulisaidia Shirika la Nyumba kuondokana na mlolongo wa kodi zinazofanya nyumba zake kuwa ghali.Waziri Lukuvi pia alisema Wizara inaanzisha mfumo wa uratibu na usimamizi wa Ardhi nchini ili kuondoa kero na ubabaishaji katika sekta ya ardhi. 2
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Bw. David Shambwe akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ya mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu Jijini Mwanza.
3
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC eneo la Buswelu Jijini Mwanza.Katika hotuba yake amesema Serikali inakusudia kuondoa kodi ya VAT kwenye uuzaji wa nyumba mpya zinazojengwa na NHC ili kuzifanya nyumba hizo kuwa nafuu.
4
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka jiwe la msingi kwenye nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa UUendelezaji Biashara wa NHC Bw. David Shambwe aliyemuakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NHC.
5
Mafundi ujenzi nao walifurahia kwa kupata fursa ya kupiga picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipokutana nao wakati wa uwekaji jiwe la msingi eneo la Buswelu.
6
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua masijala ya Ardhi ya Nyamagana kuona namna kumbukumbu za wateja zinavyotunzwa. Alishauri kumbukumbu hizo kuboreshwa ili zitumike kama msingi wakati wa utekelezaji wa mfumo mpya wa uratibu na usimamizi wa Ardhi nchini unaotarajiwa kuanza kutumika.
7
Wananchi waliofika katika Manispaa ya Nyamagana kumsikiliza na kumpa kero zao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi. Zaidi ya wananchi 100 waliweza kuwasilisha kero zao kwa Waziri na ameunda Kamati ya watendaji wa Wizara kuchambua na kufutailia kero hizo ili kuzipatia ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja.
8
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiwapa wananchi na Maafisa watendaji wa Mitaa kadi ya mawasiliano ili waweze kufahamu majibu ya malalamiko ya yao baada ya uchambuzi kukamilika.
9
Msururu wa wananchi wanyonge uliofika kumuona na kuwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi Manispaa ya Nyamagana.
10
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa tamko la kumsimamisha kazi Afisa Ardhi wa Manispaa ya Nyamagana Bw. Otieno ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za kudanganya taarifa za mteja kwa kumsomea Mh. Waziri barua na kuficha baadhi ya maandishi yaliyokuwa katika barua hiyo.
11
Watendaji mbalimbali wa NHC na Manispaa ya Ilemela wakimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu, Mwanza.
12
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ya mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC eneo la Buswelu jijini Mwanza.
13
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu Mwanza kabla ya kuweka jiwe la msingi mwishoni mwa wiki.
14
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Watendaji wa Wizara ya Ardhi na NHC wakiwa kwenye kikao katika Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza ili kujadili masula mbalimbali ya Wizara na NHC ya kuongeza ufanisi wa kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI