ZITTO KABWE AJIUNGA RASMI NA CHAMA CHA ACT-TANZANIA


Chama cha ACT-Tanzania leo kimemtangaza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe kuwa mwanachama mpya wa chama hicho kuanzia.

Zitto amesema ameamua kujiunga na chama hicho kwa kuwa ni chama chenye misingi bora ya uongozi na hivyo yeye kama kiongozi ameamua kwenda huko kwani anaamini kuwa Chama hicho ndicho kitakacholeta mapinduzi ya kweli kwenye siasa.

Mbali na Mh. Zitto Kabwe,wengine waliojiunga na chama hivyo ni pamoja na hao waliopo kwenye orodha hiyo hapo chini.
Orodha ya waliojiunga na Chama cha ACT-Tanzania leo.
Aliekuwa Mbunge  wa Jimbo Khamisma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania,katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena,Jijini Dar es salaam.kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda.Picha zote na Othman Michuzi.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007184 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda.
 Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda akionyesha kipeperushi cha Chama chao mbele ya waandishi wa habari wakati wa kumtangaza mwanachama wao mpya ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Selemani Msindi "Afande Selle" akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kuungana na Mh. Zitto Kabwe kujiunga na chama ACT-Tanzania kutokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba na kushoto ni rafiki wa Afande Selle ambaye nae amejiunga na Chama hicho,Adam Shanzy.

Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba akimkabishi kadi ya uwanachama,Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Selemani Msindi "Afande Selle" ambaye amejiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe.
 Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba pamoja na Zitto Kabwe wakinukuu kwenye makaratasi maswali mbali mbali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano wao uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena,Jijini Dar es salaam.

 Sehemu ya Wanahabari wakifatilia kwa makini hotuba ya Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe,wakati akitangaza kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania.
  Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba akiteta jambo na Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe,Zitto Kabwe
 Sehemu ya Wanachama wa ACT-Tanzania pamoja na Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mkutano huo leo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI