CHADEMA MORO KUMUUNGA MKONO ABOOD

 Mvutano wa uendelezaji ujenzi wa kituo cha mabasi cha Msamvu mjini hapa, umeingia hatua mpya baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza maandamano kuunga mkono hatua za Mbunge wa Morogoro Mjini, Aziz Abood kuhoji matumizi ya fedha za mradi huo.
Mradi huo wa ujenzi wa stendi ya mabasi unaofanywa kwa ubia na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF) Sh720 milioni zimeshatolewa kumlipa fidia aliyejenga ghorofa ndani ya eneo hilo.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro, James Joel alisema wanakusudia kufanya maandamano Aprili 14 .
Alisema uamuzi wa kufanya maandamano unatokana na Abood kufanya ziara ya kawaida kukagua mradi huo unaofanywa kwa ushirika na Manispaa ya Morogoro ambayo imeshindwa kutoa taarifa za matumizi hayo.
Mwenyekiti huyo wa Chadema, alisema kuwa katika mradi huo inaonekana kuna harafu ya ufisadi miongoni mwa viongozi wa manispaa ndiyo maana wanakataa kuweka wazi taarifa za mradi huo. “Tunaomba polisi ituache, haya maandamano ni ya amani...tunataka maelezo ya hizi fedha kwa kuwa fedha ni za wananchi, wanakosa huduma muhimu kutokana na mradi huo,”
Alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, Abood alisema kinachotakiwa ni kuwekwa wazi suala la fedha za mradi huo.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwenendo wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, Dk Albanie Marcossy alisema maandamano hayo ni mwendelezo wa operesheni iliyoanzishwa na Chadema ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi mbalimbali ya fedha za Serikali.
Katibu wa Chadema, Wilaya ya Morogoro, Esther Taweta alisema chama hicho kipo kwa ajili ya kutetea masilahi ya wananchi.
Alisema fedha zilizotolewa kujenga mradi wa maendeleo hazijulikani zilipo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI