CHUO KIKUU HURIA HUTUMIA FURSA ZILIZOPO KATIKA KUHAKIKISHA WANAKUWA WABUNIFU KUPATA VYANZO VYA MAPATO- DKT MSENGI

01
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria  cha Tanzania Prof Tom Mbwete akitoa neno la shukurani  Mkoani Katavi  wakati wa hafla fupi ya kuagwa na wanafamilia wa Chuo hicho tawi la Mkoa wa Katavi katika Hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo hicho
02
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi  katikati anayefuatia kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyemaliza muda wake akibadilishana mawazo na Viongozi wa Mkoa  wa Katavi wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo hicho mjini Mpanda.
03
.Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi  katikati anayefuatia kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyemaliza muda wake akibadilishana mawazo na Viongozi wa Mkoa  wa Katavi wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo hicho mjini Mpanda.
04
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof.Tom Mbwete mwenye suti ya blue wa pili kulia akiwa katia picha ya pamoja na Mkuu wa Mkuu wa wilaya ya Mpanda aza Mwamlia wapili kutoka mwisho kulia wakwanz kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mpanda Yusuph Ngasa mwenye suti nyeupe.mwisho ni  rais wa serikali ya wanachuo Papius Yachistwi.
……………………………………………………………………………
Na Kibada Enest Kibada-Katavi
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi ameshauri  Uongozi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Mkoa wa Katavi kuwa wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato kuliko kutegemea Ada ya wanafunzi  na ruzuku ya serikali  katika  kujiendesha kuliko kutegemea pato moja tu ambalo ni ada ya wanachuo.
Ametoa rai hiyo wakati akihutubia Jumuiya ya wananchuo na wananchi waliofurika kwenye ukumbi wa chuo hicho kwa ajili ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof,Tom Mbwete aliyemaliza muda wake kukiongoza chuo hicho.  na  sasa anakwenda kuhudumia maeneo mengine katika nchi za Bara la Afrika.
Dkt Msengi amesema uongozi wa Chuo Kikuu Huria  Mkoani humo utumia fursa zilizopo katika Mkoa  kuhakikisha wanakuwa wabunifu kupata  vyanzo vya mapato,ambapo wamepata eneo la kujenga Chuo akashauri waweke miundo mbinu itakayoasaidia kukiingizia chuo mapato kama kujenga kumbi kubwa zitakazotumika  kwa ajili ya mikutano  mbalimbali,pamoja na kumbi za semina kwa wanafunzi ,na pengine watu kutoka nje wanaweza kuja kukodisha na kuweza  kukiingizia Chuo  mapato.
Awali Meneja wa Chuo hicho tawi la Katavi Newton Kyando  ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo hicho alieleza  kuwa chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo na ukata wa fedha, mwamko mdogo wa elimu miongoni mwa baadhi ya wananchi Mkoani  humo katika  kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu huria,pamoja na uchache wa watumishi katika tawi la Katavi.
Changamoto nyingine alieliza kuwa ni ukosefu wa maktaba pamoja na upungufu wa watumishi  pamoja  na uchache wa fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya uendeshaji  ambapo fedha inayoletwa ni ndogo ambayo haitoshelezi uendeshaji wa ofisi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria anayemaliza muda wake  Prof Tomu Mbete akitoa neno la shukurani kwa wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria tawi la Katavi aliwashukuru kwa juhudi zao  za kukifanya chuo hicho kiweze kuwa na wanafunzi na wananchi mkoani humo wameonekeana kuwa na mwamko wa kukitumia kujipatia elimu.
 Prof Mbwete akaeleza kuwa kwa sasa anaenda kutumikia wananchi wengine wa Afrika katika nchi ya Cameruni ambapo anaenda kuongoza Chuo cha Umoja wa Afrika Pan Afrikanism ambapo makao yake yako Yaunde Cammeruni hivyo atakuwa huko.
Pia katika hatua nyingine alifurahishwa na zawadi walizompatia kutoka Mkoa wa katavi akazielezea kuwa  ni moja ya zawadi ambazo ni bora kati ya zawadi alizopewa,katika maeneo mbalimbali aliyopita kuagwa na wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria kwenye matawi yake yote.
Prof.Mbwete akizungumzi fursa zilzopo kwanza alishukuru kumaliza  muda wake bila kusikia mgomo wa aina yeyote na hajawahi kusikia wanafunzi wala mwanafunzi  yeyote katika kpindi cha miaka kumi aliyoongoza wakigoma  hata kama wana matatizo ni watu wenye  kuvumilia na wako  tofauti na vyuo vingine.
Akizungumzia  kuhusu ujenzi wa  Chuo Kikuu Huria tawi la Mkoa wa Katavi  ameleza kuwa  eneo lililopatikana amesaidia kuweza kununua ambapo jumla ya shilingi milioni 45 zimemika ameitoa mwenyewe kwa ajili ya kusaidia kuweza kulipa fidia  eneo lile ambalo yalikuwa mashamba ya watu,akasisitiza eneo hilo lipimwe na kupatiwa hati ili ujenzi uanze.
Akaeleza kuwa iwapo litamilikiwa na Chuo litaweza kutumika  kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa ya chuo,nyumba za walimu,pamoja ,makitaba ya kisasa na kumbi nzuri za mikutano  ambazo wanafunzi watakuwa wanafanyia semina na makongamano,pia wananchi wakihitaji watakuwa wanakodishiwa na kukiingizia chuo mapato.
Pia Chuo kimeanzisha College za Mikoa na Vituo Wilayani ili kusaidia kuwapatia eleimu wananchi walio wengi,kwa upande wa Mkoa wa Katavi ni moja ya mikoa inayofanya vizuri hususani katika darasa la TEHAMA Kwani kila mwaka wanafunzi wanaongezeka kwa kasi tofauti na Mikoa mingine.
 Kuhusu  Vituo vya  Mikoa ya Katavi na Katavi  ameeleza kuwa mikoa hiyo inaingizwa kwenye mkongo wa Taifa,iwapo mikoa hii ikingia katika mkongo wa Taifa wanachuo watanufaika   sana kwa kujisomea na kpatiwa materiali kupitia kwa njia ya matndao.
 Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho katika risala yao iliyosomwa na Rais wa wanachuo Yachitu ilieleza kuwa Makamu wa Chuo Prof Mbwete ni mfano wa kuigwa kwa jinsi alivyo mbunifu kiongozi hodari ,mchapakazi na anayependa kusikiliza na kuendelea kujifunza na anayependa kupokea ushauri kuondoka kwake ni pengo ambalo litachukua muda kuliziba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*