HABARI MPASUKOOO!!!!!!!!!!!!!!!! MABOMU YA MACHOZI YANAPIGWA SASA KUWATAWANYA MADEREVA WALIOGOMA UBUNGO DAR

Mtafaruku mkubwa umetokea muda huu katika Kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo, na Barabara ya Morogoro, baada ya polisi kupiga mabomu kwatawanya madereva, makondakta wa daladala  na mabasi na madereva wa malori waliogoma kuishinikisha Serikali kupunguza gharama ya kwenda kusomea taaluma hiyo.

Kupigwa kwa mabomu hayo kumesababisha watu wakiwemo abiria kukimbia ovyo ili wasipatwe na zahama hilo.

Waliogoma wanaendelea kupiga mawe daladala, mabasi , na vyombo vingine vya moto vinavyoendelea kubeba abiria.

Kwa ujumla usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umekuwa mgumu baada ya baadhi ya wamiliki wa magari hasa daladala kutoruhusu magari yao kuingia barabarani kuhofia magari yao kuvunjwa na watu hao wenye hasira.

Walioitisha mgomo huo hawakubaliani na ada kubwa ya sh. 550,000  iliyowekwa na serikali kwa ajili ya mafunzo ya udereva. Lakini Serikali imesema madai hayo ni ya uongo ni uvumi tu unaoenezwa . 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.