KOMREDI KINANA AMALIZA ZIARA YA KM 7312 KATIKA MIKOA YA DODOMA, ARUSHA NA KILIMANJARO

 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinanaukilakiwa na waendesha Bodaboda mjini Moshi ulipowasili kutoka Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara ya mikoa mitatu ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, amezunguka kwa magari katika mkioa hiyo kwa umbali wa Km 7312, ametembelea wilaya 19, Majimbo 25. Amefanya jumla ya mikutano 216 na amevuna wanachama wapya 18,119 ambapo Chadema ni wanachama 2442 na amekagua jumla ya miradi ya maendeleo 179.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Waendesha Bodaboda wa Mjini Moshi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM,Komredi Kinana alipokuwa akiwahutubia katika Stendi Kuu Mjini Moshi. Ameahidi kuwaandalia utaratibu wa kuwakopesha pikipiki.
 Wanyabiashara wa Soko la Kati Mjini Moshi wakiwa na mabango walipouzuia msafara wa Komredi Kinana wakitaka awapatie suluhu ya kufunguliwa soko lao lililofungwa na Manispaa mwaka mmoja uliopita kwa madai ya ukarabati.
 Nape akiwapooza wafanyabiashara hao ili watoe kilio chao kwa Komredi Kinana
 Komredi Kinana na Nape wakikagua soko hilo
 Komredi Kinana akizungumza na wafanyabiashara hao
 ndani ya soko ambapo aliagiza Mkuu wa Mkoa  huo, Leonidas Gama alipatie ufumbuzi wa haraka ili ilifunguliwe

 Kinana akilakiwa na kikundi cha akina mama cha Kiurashi kinachotengeneza nguo za batiki
 Komredi Kinana akizungumza na Kikundi cha Vijana wafyatua matofali cha  cha Inter Lockin blocks mjini Moshi
 Komredi Kinana akilakiwa na akina mama lishe Kata ya Njoro
 Wanachama wa CCM wa wakiangalia picha walizopiga wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana katika Kata ya Njoro
 Mjumbe wa NEC,Taifa, Agrrey Marealle akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mandela, eneo la Bomambuzi, Pasua, Moshi Mjini
 Baadhi ya wananchi nwakisikiliza hotuba katika mkutano huo wa hadhara. Aliyevaa gauni la kitenge mstari wa mbele ni Beatrice Shirima ambaye ni  Mwenyekiti wa UV CCM Wilaya ya Rombo, ambaye pia ni  Ofisa wa CCM Makao Makuu.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akienbdesha gari la zamani lililokarabatiwa na VETA, ambalo liliwahi tumiwa na Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere katika harakati za kudai uhuru. Gari hilo litahifadhiwa katika Makusho ya Taifa Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA