MBUNGE MGIMWA AJITOLEA KUANZA UJENZI WA DARASA KUBWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA IFUND


Mbunge  wa  jimbo la kalenga  Godfrey  Mgimwa  akishiriki  kucheza  kwaito na wanafunzi wa  shule ya  sekondari ya  wasichana Ifunda  leo

Mkuu  wa  shule ya  sekondari ya  wasichana  Ifunda akimpongeza mwalimu  wa kujitolea  wa Hesabu Shuleni  hapo  mbele ya  mbunge Godfrey Mgimwa
Mbunge  wa Kalenga  Godfrey Mgimwa kushoto  akikavbidhi  zawadi  kwa  walimu  wa  shule ya  sekondari ya  wasichana Ifunda
Wanafumnzi  wa  kidato cha  sita  wakikabidhiwa  vyeti  na  mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa
Wanafunzi  wa  shule ya  sekondari  ya  wasichana  Ifunda  wakimpokea  mbunge  wa  jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa kwa  gwalide  maalum
Mbunge  Mgimwa wa tatu  kulia  akiongozana na mwenyekiti wa bodi  ya shule hiyo  Abed  Kiponza  kulia na viongozi mbali mbali wa  shule  hiyo ya  serikali ya  kijiji  cha Ifunda
Mbunge  Mgimwa  akivishwa  skafu 
Mbunge  Mgimwa  akitazama  mwanafunzi  wa  Ifunda akimpasua Simbilisi 
Baada ya  upasuaji  kufanyika
Mwenyekiti  wa bodi ya  shule ya  sekondari ya  wasichana  Ifunda Abed  Kiponza akimpongeza mbunge Mgimwa
Mbunge  Mgimwa  akiwahutubia  wanafunzi  na  wazazi
 Na MatukiodaimaBLOg
BAADA ya  wanafunzi kukosa darasa  kubwa la  kusomea ,mbunge   wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa amejitolea kuanza ujenzi  wa darasa  hilo kuahidi kuchangia   mifuko  200  ya  Saruji  yenye  thamani ya  zaidi ya Tsh milioni 3 kwa  ajili ya  kusaidia  ujenzi  wa  darala litakalotumiwa na  wanafunzi  zaidi ya 200 katika  shule ya  sekondari  ya wasichana  Ifunda  katika  wilaya ya Iringa   mkoani  Iringa.

Mbunge   Mgimwa ambae  alikuwa  mgeni  rasmi  katika  mahafali ya  9  ya  shule   hiyo  ametoa ahadi   leo   kufuatia  maombi ya  uongozi  wa  shule   hiyo  .

Alisema  kuwa lengo lake  kuona  kiwango  cha  elimu  katika  jimbo lake  kinaendelea  kukua  zaidi na  ndio  sababu  ameendelea  kusaidia  ujenzi  wa maabara pamoja na  kuchangia shughuli  mbali mbali  za  kimaendeleo zinazofanywa na  wananchi  wake  zikiwemo  za ujenzi  wa  shule ,nyumba  za  walimu pamoja na  ujenzi  wa maabara zinazojengwa kufuatia  agiza  la   Rais  Dkt  Jakaya  Kikwete.

"Leo  hapa  nimeelezwa  changamoto   mbali  mbali  zinazoikabili  shule  hii  kwanza  juu ya  uchakavu  wa majengo ,uhaba  wa  walimu  wa masomo ya  Hisabati na  Sayansi lakini  pia  ukosefu  wa darasa  kubwa  litakaloweza  kuchukua  wanafunzi  200  kwa  wakati mmoja  na mmeomba  kusaidiwa   kati ya  bati 200 ama  Saruji  .......sasa   ili  ujenzi  huu  uanze mimi  nitachangia saruji  mifuko  yote  200  ila rai yangu  kwa  wazazi tuungane  katika  ujenzi  huu"

Kuhusu tatizo la  uhaba  wa  walimu  alisema  kuwa  hiyo ni  changamoto  ya  nchi  nzima  japo  alisema  lazima  atalifikisha kwa  mkurugenzi mtendaji wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Iringa  ili  kuweza  kuitazama  shule   hiyo  kwa  jicho  la tatu  .

Pia  mbunge   huyo  alisema  kuwa  toka  ameingia  madarakani mwaka  jana  kuna baadhi ya  kazi  kubwa  amepata  kuzifanya katika  jimbo  hilo  na  kuwa   wananchi  wa  jimbo  hilo  ni mashahidi  katika suala  hilo na  kuwa akiwa  kama mwakilishi  wa  wananchi  wa Kalenga atahakikisha kwa  muda  uliobaki kuona anatafuta  majibu ya  changamoto mbali mbali  za  jimbo  hilo.

Aidha  mbunge  huyo  aliupongeza  uongozi  wa shule  hiyo kwa kazi nzuri ya  ukuzaji  wa taaluma  shuleni hapo na hata  kuifanya  shule   hiyo  kuwa  moja kati ya  shule  zenye sifa  nzuri ya  kufaulisha ndani ya  wilaya ya  Iringa ,mkoa na taifa   na  kuwataka   wahitimu  wa  kidato cha  sita  kutumia  muda  uliobaki kujisomea  zaidi  ili  kuendeleza  rekodi ya  kufaulu  vema  katika  mitihani ya kidato  cha sita.

Mwenyekiti  wa  bodi ya  shule  hiyo  Abed Kiponza akimshukuru  mbunge  Mgimwa  alisema  kuwa msaada  huo  ni  ukombozi  mkubwa wa maendeleo ya  ujenzi  wa  darasa  hilo   pia  aliwaomba  wazazi na  wadau mbali mbali  kujitolea  kushiriki  ujenzi  wa  darasa  hilo  pamoja na uboreshaji  wa majengo  ya  shule  hiyo .

Kiponza  alisema  kuwa  shule  hiyo  ni   shule  ambayo  imekuwa  ikiendeshwa  kwa misingi  bora ya  kitaaluma na  kuwa  haijapata  kuwa na mgomo  wa  wanafunzi  wala  walimu  tofauti na  shule  nyingine .

Mkuu  wa  shule   hiyo  Bi Zaina  Salingwa katika  taarifa  yake  kwa wazazi na  mgeni  rasmi  alisema  kuwa  shule   hiyo  ilianza mwaka 2005  baada ya  kufungwa kwa  kilichokuwa  chuo  cha ualimu  Ifunda na  kuwa hali ya majengo  hayo ni chakavu  zaidi  baada ya majengo hayo  kujengwa  toka mwaka 1985.

Alisema  kuwa  shule  hiyo ni  shule ya  bweni  yenye  uwezo  wa  kuchukua  wanafunzi 640  lakini ina  wanafunzi 653  wakiwepo  wanafunzi 440  wa  kidato cha tano na wanafunzi 213 wa kidato cha sita na  kuwa asilimia 90 ya  wanafunzi  wanasoma  masomo ya  Sayansi na jumla ya  michepuo  waliyonayo  ni  saba   yani CBG, PCB, PCM, PGM,EGM,HGK na HGE na  kuwa  walimu   waliopo  ni 23 huku masomo ya Sayansi  na  Hesabu  yakiwa hayana  mwalimu hata  mmoja  zaidi ya  kukodi  walimu  kutoka nje.

Mkuu   huyo  alisema  kuwa hadi sasa  shule   hiyo  imefanikiwa  kuwa na gari la  mkuu  wa  shule  ambalo limenunuliwa kwa  kiasi  cha Tsh milioni 20   fedha  zilizochangwa na  wadau mbali mbali  akiwemo kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa  Salim Asas .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA