MEMBE ASEMA HAKUNA MTANZANIA ALIYEUAWA KATIKA VURUGU AFRIKA KUSINI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mauaji ya raia wa kigeni yanayoendelea nchini Afrika Kusini, ambapo alisema hakuna Mtanzania aliyeuawa katika sakata hilo. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Membe ambaye amemwita Balozi wa Tanzania n chini Afrika Kusini, Msuya, kuelezea hali inavyoendelea nchini humo, alisema kuwa taarifa waliyonayo ni kwamba Watanzania 23 ni miongoni mwa raia wa kigeni zaidi ya 300, waliohifadhiwa kwenye kambi maalumu kwa ajili ya ulinzi wasizulike na vurugu hizo.

Alikanusha habari ziliozagaa kwenye vyombo vya habari kwamba watanzania watatu wamefariki kwenye vurugu hizo. Alisema kuwa watu hao walikufa kwenye matukio mengine, ambapo mmoja amefia gerezani kwa kuchomwa kisu, mwingine alipigwa risasi akishiriki katika kitendo cha wizi na mwingine alikuwa amelazwa hospitali kwa ugonjwa.

Watanzania 21  wanahifadhiwa katika Kambi hiyo,watarejeshwa nchini, isipokuwa wawili waliokataa kurejea. Alisema kuwa hadi sasa maofisa wa ubalozi wetu Afrika Kusini, tayari wameshapelekwa Jiji la Durban na Johannesburg kucheki hali watanzania. Inakadiriwa kuwa zaidi ya Wata nzan ia 10,000 Wanaishi Afrika Kusini.

Amewataka watanzania waote wanaokwenda kihalali na wanaokwenda Afrika Kusini kwa njia ya panya wafanye utaratibu wa kujisajili Ubalozi wa T anzania nchini humo, ili wanapopatwa na matatizo iwe rahisi kuwasaidia.

Alisifu juhudi zinazofanywa sasa na Serikali ya Afrika Kusini ya kurudisha utulivu, hasa kwa kumtumia Chifu wa Kabila la Wazulu, kuwakataza vijana kuendelea na vurugu. Inadaiwa chifu huyo ndiye alikuwa mhamasishaji mkubwa vurugu hizo ambazo chanzo chake kikubwa ni kuilaumu Serikali ya nchi hiyo kuruhusu ajira kwa raia wa kigeni kitendo ambacho wanadai kinapunguza ajira kwa upande wa wazawa.
 Membe akiingia kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam kuzungmza na wanahabari. Kushoto ni mlinzi wake na kulia ni Katibu Msaidizi wake.
 Membe akizungmza katika mkutano huo
 Wanahabari wakiwa kazini
 Membe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Msuya.
 Mwandishi wa Habari wa The Citizen, Mkinga Mkinga akuliza swali wakati wa mkutano huo

 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Suleiman Msuya akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
 Membe akielezea historia ya vurugu hizo ambazo kabla ziliwahi tokea tena 2008 Afrika Kusini
Membe akiondoka  huku akiwa na wanahabari pamoja na maofisa wa wizara yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI