MKUU WA MKOA WA TANGA AITISHA KIKAO KUWEKA MIKAKATI YA KUIOKOA COASTAL UNION

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union,Akida Machai akimuelezea mikakati ya timu hiyo mkuu wa Mkoa waTanga Magalula Saidi wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa Coastal Union na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo
ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao
iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati
alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana
ambapo Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa
viongozi wengine kwenye kikao hicho.

Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza
kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na
madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa
ligi nyengine.

Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano
iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa
maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto
alimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa
maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio..

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai
alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia
kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo
iliyosalia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid
Abdallah.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.