Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas
Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa
Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania
na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi
wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold
Mahona.
Viongozi wa chama hicho wakiwa meza
kuu. Kutoka kushoto Kaimu Katibu wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam,
Peter Katunka, Kaimu Katibu Mkuu, Leopold Mahona, Mwenyekiti, Kadawi
Lucas Limbu na Katibu Muenezi Fredy Kisena.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu (kulia) akisisitiza jambo.
Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for
Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia
Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai
ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa
ACT-Wazalendo.
Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.
"Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa
kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika
kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho.
Comments