NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI CHARLES KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

      

1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na  Kaimu Katibu Mkuu  wa Wizara  ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye  ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi  tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto  katika utendaji  kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
2
Mwenyekiti  wa Chama cha Wafanyakazi wa  Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara  ya Nishati na Madini, Marcelina  Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava  (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
3
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa Wizara  ya Nishati na Madini  wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani)
4
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Ngosi  Mwihava (kulia)  akisoma hotuba ya kumkaribisha  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
5
6
Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
8
Baadhi  ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara  ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina  la “solidarity forever
9
Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara  ya Nishati na Madini, Michael Marandu (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua mkutano huo.
10
Naibu  Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga  (katikati, waliokaa mbele) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara ya Nishati na Madini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*