Skip to main content

NHIF yazindua awamu ya pili ya Kampeni ya uhamasishaji Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)


1
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA)
2
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akiangalia mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga afya ya jamii CHF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.
3
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya jamii CHF.
4
Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na afya ya Jamii CHF.
6
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF na madaktari wakiandaa eneo la kuhudumia wananchi kwa upimaji wa afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.
7
Baadhi ya wanahabari Othman Michuzi wa Michuzi Media na Fatuma kutoka Clouds Lindi wakipata taswira mbalimbali katika uzinduzi huo.8
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF.
10
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF na katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond.
11
Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi wilaya ni Kilwa.
12
Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF.
13
Baadhi ya madaktari wakisubiri kuanza kutoa huduma katika uzinduzi huo.
14
Wananchi wakipima uzito.
15
Madaktari wakiwachunguza na kuwapima afya wananchi wa kijiji cha Njia Nne kata ya Tingi wakati wa uzinduzi huo.
16
Wasanii Shoti na Faida wakiburudisha wananchi huku wananchi hao wakiendelea kupata huduma katika uzinduzi huo.
17
Wananchi wakiendelea kupima afya.
18
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi huo kutoka kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Salvatory Okum Afisa Mfuko wa Afya ya Jamii, Fortunata Raymond Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi na Paul marenga Afisa Matekelezo na Uendeshaji NHIF mkoa wa Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Bw Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatikana muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani Kilwa.
Ulega alisema serikali kupitia mifuko ya uchangiaji ya bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.
Awali, mkurugenzi wa masoko na utafiti wa bima ya afya Rehani Athumani alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa kampeni hiyo inayozinduliwa itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasisha nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.
Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.
Naye mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa mifuko ya afya ya jamiii nchini (TNCHF) bibi Kidani Mhenga amewaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi ya Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia mfuko wa afya wa jamii katika mikoa hiyo.
Ameomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.
Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU