Bondia nyota, Manny Pacquiao amesema mchezo wa ngumi ni kati ya michezo bora kabisa duniani.


Pacquiao amesema mchezo huo umebadilisha maisha ya wengi na mara nyingi amekuwa akikumbuka alivyoishi maisha ya shida huku mama yake akihangaika kusaka fedha ya chakula.

“Lakini leo napata kila kitu, familia yangu inaishi kwa raha. Ni mchezo ambao kwa juhudi zako mwenyewe ndiyo unavyoweza kupata malipo.

“Najiandaa vizuri, najua nitapambana na lakini Mayweather awe makini, ile hamu yangu ya ushindi, hamu ya kutaka kummaliza mtu imerejea,” alisema.

Mayweather na Pacqioa watapanda ulingoni Mei 3 kwa saa za Afrika Mashariki katika pambano ghali zaidi katika mchezo wa ngumi duniani.


Tayari kila mmoja amekuwa akiendelea na mazoezi huku akionyesha mbwembwe za kila aina.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*