RAIS AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA

http://media.silive.com/opinion_columns/photo/mohamed-morsi-ec654788db781ebf.jpgRais wa Zamani wa Misri, Mohammed Morsi. 
Makahama nchini Mirsi imemhukumu aliyekuwa rais wa zamani Mohammed Mosri kifungo cha miaka 20 gerezani kutokana na kuuawa kwa waamdamanaji wakati akiwa madarakani. 


Hii nidyo hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani na jeshi la nchi hiyo mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.

Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka 2012.

Wakati umati ulipokusanyika nje ya Ikulu, Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo. Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye makabiliano, wengi kutoka Muslim Brotherhood.

Kabla ya kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha kuhalalisha utawala wake kwa kumkandamiza Morsi. Mara baada ya hukumu hiyo, chama cha Muslim Brotherhood kimeitisha maandamano kote nchini humo hali iliyosababisha makabiliano makali na polisi.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, rufaa ya hukumu hiyo iko wazi na mshitakiwa anaweza kufanya hivyo. Mohammed Morsi ndiye rais wa kwanza katika Taifa hilo kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia baada ya kuangushwa utawala wa muda mrefu wa Hosni Mubarak na waandamanaji, lakini ulidumu kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuangushwa na jeshi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.