SERIKALI YAANZA KUTATUA MIGOGORO KWA WANANCHI DHIDI YA HIFADHI ZA TAIFA.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akiongea na waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa Habari Ukiendelea

SERIKALI imeazimia kumaliza migogoro yote ambayo ipo kwa wananchi ambapo Wizara ya maliasili na utalii imeanza kuihesabu ili itatuliwe mapema iwezekanavyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi(CCM).
 
Hayo yalibainishwa na, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumaliza ziara yake wilayani Mbarali, ambapo alisema Serikali imeona ianze upya kufuatilia suala hilo ikiwa ni pamoja na kutatua mgogoro uliopo.
 
Waziri Nyalandu alilazimika kufanya ziara Wilayani Mbarali kufuatia kuwepo kwa mgogoro wa wananchi wa vijiji 21 kugomea kupisha hifadhi ya Ruaha.
 
Waziri Nyalandu alisema uamuzi wa kuvihamisha vijiji hivyo ili kupanua hifadhi ya Ruaha ulitokana na tangazo la Rais (GN28) la kuifanya eneo la Ihefu na vijiji vinavyoizunguka kuwa sehemu ya hifadhi.
 
Alisema mgogoro huo ulianza mwaka 2009/2010 baina ya Usangu game reserve na bonde la Ihefu kwenda Ruaha ambapo wakazi wa maeneo hayo ambao walipangwa kuhama walitengewa fidia shilingi Bilion 4 na baadaye kuongezwa Bilion 3 na kuwalipa fidia jumla ya Bilion 7.
 
Alisema baada ya hapo mgogoro ulitokea kwa baadhi ya wananchi kudai kulipwa tofauti na makadirio, wengine kudhurumiwa kabisa  hivyo Serikali imeona wananchi hao wasiondoke kwanza hadi madai yao yahakikiwe kwanza ambapo madai yote yanatarajiwa kuanza kulipwa Julai 1, mwaka huu.
 
Aliongeza kuwa mgogoro huo umetokana na tangazo la serikali kuandaliwa tofauti na matakwa ya wananchi, pia maeneo yalioyoagizwa yakawa tofauti na maeneo yaliyoorodheshwa  ambapo maeneo ya awali hayakuguswa kabisa.
 
Waziri Nyalandu alisema kutokana na hali hiyo, wananchi hao hawataondolewa katika maeneo yao bali timu mbili zimeundwa ili kuchunguza sakata hilo.
 
Alisema timu ya kwanza itafuatilia madai yote kisha watayapeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye atayawasilisha wizarani kwa ajili ya utekelezaji.
 
Alisema timu ya pili itakuwa ya wataalamu wa Ikolojia ambao wataangalia mfumo wote wa ekolojia na maji na namna ya kutatua mgogoro ili wananchi wawe sehemu ya hifadhi pamoja na kuangalia namna maji yasiharibu mto Ruaha Mkuu.
 

Aidha alitoa wito kwa Wananchi kuacha kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi ya Ruaha mkuu bali wanapaswa nao kuwa sehemu ya uhifadhi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI