TANZIA: CHIGWELE CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA


Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za asili nchini, Chigwele Che Mundugwao amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya damu.
Marehemu Chigwele Che Mundugwao amewahi kulipatia taifa sifa kimataifa katika nchi za Scandinavia ambako alijipatia mialiko mbalimbali ya kuwaburudisha mashabiki wake wa muziki.
Miongoni mwa bendi ambazo amewahi kuimbia ni pamoja na Tatu Nane.
Marehemu Che Mundugwao aliyezaliwa mwaka 1968 amefariki akiwa na umri wa miaka 47.
UNDANI WA CHE MUNDUGWAO
Chingwale Che Mundugwao  (47) hadi anapatwa na umauti alikuwa mahabusu…
Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za asili nchini, Chigwele Che Mundugwao amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya damu.
Marehemu Chigwele Che Mundugwao amewahi kulipatia taifa sifa kimataifa katika nchi za Scandinavia ambako alijipatia mialiko mbalimbali ya kuwaburudisha mashabiki wake wa muziki.
Miongoni mwa bendi ambazo amewahi kuimbia ni pamoja na Tatu Nane.
Marehemu Che Mundugwao aliyezaliwa mwaka 1968 amefariki akiwa na umri wa miaka 47.
UNDANI WA CHE MUNDUGWAO
Chingwale Che Mundugwao  (47) hadi anapatwa na umauti alikuwa mahabusu akikabiliwa na kesi ya wizi wa hati za kusafiria 26 (Passports) mali ya serikali tangu aliposhitakiwa rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Juni 2, 2013, akiwa na wenzake 8.
 Washitakiwa wengine ni  wahudumu wa Idara ya Uhamiaji Adam Athuman na Abdallah Salehe. Raia wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa  Ugavi wa  Idara ya Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi  cha Zimamoto na Uokoaji, mfanyabiashara  Ally Jabir, Rajab Momba na Haji Mshamu.
 Makosa waliyokuwa wakishitakiwa nayo yalikuwa na dhamana lakini Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwendendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , aliwanyima dhamana hivyo kusota gerezani kwa kipindi chote hicho hadi Che alipougua maradhi ya damu na kupelekwa hospitali ya Taifa ambako alipatwa na mauti baada ya kulazwa kwa muda mrefu. Che Mundugwao alikuwa mahabusu wa Gereza la Keko jijini Dar es salaam . 
 Aidha, wakati akiwa gerezani, Che Mundugwao alifiwa  na mtoto wake lakini hakuweza kushiriki msiba wake kwasababu alikuwa gerezani chini ya ulinzi  na leo masikini amemfuata mwanae mavumbini!.
 Binafsi Che Mundugwao nilianza kumfahamu tangu Kipindi kile akiwa mwanamuziki wa muziki wa asili na aliwahi kupiga wimbo wake mmoja uliompatia  umaarufu unaitwa 'TUMETOKA KWETU MAHENGE....TUMEKUJA  DAR ES SALAM KUJA KUCHEZA SINDIMBA '. Mwaka 2000.
 Wimbo huu ulitamba katika miaka ya 1990 na wanamuziki waliocheza ni pamoja na Luiza Mbutu ambaye kwa sasa ni kiongozi wa Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”. Kwa mtakaoenda kutaza video ya wimbo huo mtakubaliana nami kuwa  Luiza Mbutu ametoka mbali katika fani ya muziki na amebadilika sana.
 Aidha Che Mundugwao aliendesha Kipindi cha Muziki wa Asili  Katika Redio Tumaini na hatimaye mwisho wa siku Juni 3 mwaka 2013, Mimi nilipokuwa Mwandishi wa Habari  za Mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima, nilishuhudia Che Mundugwao akipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mchana, akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu na kupandishwa kizimbani na kushitakiwa kwa kesi hiyo.
 Nilisikitika sana  kuona Che Mundugwao yuko mikononi mwa dola na nilikuwa sina jinsi ya kumsaidia kwa sababu licha ya kuwa ni rafiki yangu sikua na cha kumsaidia, Sheria ni Msumeno!
 Mungu aiweke roho ya marehemu mahali panapostahili. Amina.
(Stori na Happiness Katabazi)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI