WATU 560 WAUAWA KWA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI NEPAL


Majengo yaliyoporomoshwa kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal.
Majeruhi baada ya kuokolewa wakati wa tetemeko hilo.

Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo Magharibi mwa Nepal karibu na Mji Mkuu wa Kathmandu .Maafisa wa polisi wamethibitisha kuwa zaidi ya watu 560 wamefariki dunia huku wengi wakiwa hawajulikani waliko na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka. 


Shirika la utafiti la Marekani limesema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane Mashariki mwa Pokhara Magharibi mwa mji Mkuu wa Kathmandu.Kuna ripoti za uharibifu wa majengo na bidhaa, makazi ya watu hata miundo mbinu ya Mawasiliano ya simu nayo yameharibiwa vibaya. 

Picha za majengo yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii. 
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Mitetemeko mingine midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*