AIBU TAIFA STARS KUFUNGWA NA TIMU ZENYE VIWANGO VIDOGO VYA FIFA

Kikosi cha Tanzania kilichofungwa  na Madagascar Kombe la Cosaf
TAREHE 21 MEI 2015
STARS YAPOTEZA MCHEZO WA PILI
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 - 0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.

Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya makundi, kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.

Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.

Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.

“Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.

Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.

Kufuatia Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.

Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.


KAMATI YA UTENDAJI YA TFF KUKUTANA MEI 24
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF inatarajiwa kukutana jumapili tarehe 24, Mei mwaka huu ikiwa ni kikao cha kawaida cha kamati hiyo.

Moja ya ajenda katika kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo, maandalizi na maendeleo ya timu zaetu za Taifa za mpira wa miguu nchini.

NB: Picha za mchezo wa jana kati ya Tanzania dhidi ya Madagascar 
zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

-- 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI