BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU (HESLB), YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2015/16


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi (HELSB) George Nyatega, akizungumza na waandishi wa habari nofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 1, 2015



Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.

Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).

Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.

“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.

Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.

Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA