HABARI MPASUKOOO!!!!!!!!MABASI UBUNGO YALAZIMISHWA KUONDOKA CHINI YA ULINZI WA POLISI

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Kituo cha Masi Ubungo, Dar es Salaam, ni kwamba mabasi ya abiria yameanza kuondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi kueleka mikoni.

Mabasi hayo yalishindwa kuondoka jana hadi leo asubuhi baada ya madereva wa mabasi hayo kuoma wakiitaka Serikali iingilie kati mgogoro wao na wamiliki wa mabasi kuhusu mikataba yao ya ajira.

 
Mabasi ya Shabiby yametoka kwa escort ya police, lakini taarifa na habari zinazoendelea ni kuwa abiria nao wanapanga ikifika saa 6 mchana wanazuia magari yote yanayopita barabara ya morogoro hususani ya serikali.


Update hii inakujua toka hapa Ubungo:
Kuna gari hapa min bus imejaa askali kanzu ambao wengine wamevaa mabomu wakishuka na wanatoa upepo wa tyres za magari.

Tayari Waziri Mkuu Kivuli, Mbowe tayari ameshafika Ubungo na kuangalia nini kifanyike, kutokana na Waziri mkuu husika kukataa.


Pia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda ameshafika katika kituo hicho, wako pamoja na Mbowe.

 Askari wakiimarisha ulinzi katika Kituo cha Mabasi Ubungo
 Basi la Shabiby likijiandaa kuondoka Ubungo asubuhi
 Baadhi ya abiria waliokwama Ubungo

Nauli za leo ni balaa:
1. Ubungo - Buguruni (Noah 1000, Bajaj 1000, Canter 500)
2. Ubungo - Mbagala (Noah 3000, Canter 2000, Bajaj 2000)
3. Ubungo- Kariakoo (Canter 3000, Noah 4000, Boda Boda 10,000 usiulize jioni kurud ubungo ni shilingj ngapi)

4. Kutoka Gongo la Mboto hadi Kariakoo Kilikuu sh. 4000

Serikali inatakiwa kufanya ufumbuzi wa haraka kuhusu mgomo huu wa madereva wa mabasi ili wananchi wasiendelee kupata adha na mateso.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA