HABARI MPASUKOOOOOO!!!!!! RAIS NKURUNZIZA WA BURUNDI AKISAKATA KABUMBU LEO

 Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana akicheza mpira pamoja na marafiki zake mjini Bujumbura licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.

 Rais Nkurunziza,alikuwa akisakata kabumbu ndani ya mji mkuu wa Bujumbura mji uliokumbwa na maandamano makubwa tangu atangaze nia ya kuwania awamu ya tatu uongozini.

 Hii leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura. 

Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.

 Walioshuhudia wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.

 Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi. 

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani.

 Katika hotuba kwenye runinga ya taifa, amesema kuwa asilimia tisini na tisa nukta tisa ya Burundi ina amani. Anasema kuwa hakuna mtu yeyote anayetaka kufufua taharuki ya kikabila.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/rais-pierre-nkurunziza-wa-burundi.html
Copyright © saluti 5
 Rais Nkurunziza ni kocha aliyehitimu

 Rais Nkurunziza alikuwa akicheza dhidi ya marafiki zake 

 Mechi hiyo ilikuwa mjini Bujumbura

Rais Nkurunziza anatimu yake ''Hallelujah FC ''

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI