Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua
makatibu tawala wa Mikoa ya Singida na Shinyanga kuanzia jana, Jumatatu, Mei 25,
2015.
Katika
uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Festo Luganda Kang’ombe kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na
Ndugu Abdul Rashid Dachi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Kabla
ya uteuzi wake, Ndugu Kang’ombe alikuwa Mkurugenzi wa Halmashuri ya Kibaha,
Mkoa wa Pwani wakati Ndugu Dachi alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Sekretarieti
ya Mkoa wa Lindi.
Ndugu
Kang’ombe anachukua nafasi ya Ndugu Liana Hassan ambaye amestaafu utumishi wa
umma kwa mujibu wa sheria tokea Machi, mwaka huu, na Ndugu Dachi anachukua
nafasi ya Ndugu Anselm Tarimo ambaye naye alistaafu utumishi wa umma kwa mujibu
wa sheria Januari 22, mwaka huu, 2015.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
26
Mei, 2015
Comments