MADAGASCAR WAITUPA NJE GHANA KOMBE LA COSAFA, WAICHAPA 2-1

MADAGASCAR imeitoa Ghana katika Kombe la COSAFA, baada ya kuichapa mabao 2-1 katika Robo Fainali ya tatu jioni ya leo Uwanja wa Royal Bafukeng Sports Palace mjini Rusternburg, Afrika Kusini. 
Ghana sasa inaungana na Zambia na Afrika Kusini kuangukia kwenye Nusu Fainali za vibonde, maarufu kama michuano ya Plate, wakati Madagascar inaungana na Botwsana na Namibia katika mbio za Kombe la COSAFA 2015.  
Madagascar walipata bao lao la kwanza dakika ya 28 kwa shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na Rhino Randriamanjaka na kumpita kipa Fatau Dauda.
Ghana wakafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 37 kupitia kwa Daniel Darkwah lililompita kipa wa Madagascar, Jean Dieudonne.
Wakati wengi wakiamini mechi itaisha kwa sare ya 1-1, Olivier Simouri akaifungia Madagascar bao la ushindi dakika ya 90.
Kikosi cha Madagascar kilikuwa; Jean Dieudonne, Njakanirina Tobisia, Fenolahy Zenith, Francois Andrianomenjanahary, Michael Rabeson, Simouri Olivier, Dina Razanakoto, Claudel Fanomezana, Lantoniaina Andriamanalina, Rinho Randriamanjaka na Martin Rakotoharimalala.
Ghana; Fatau Dauda, Godfred Saka, Malik Akowuah, Michael Akuffu, Daniel Darkwah, Joshua Tijani, Alfred Nelson, Hans Kwofie, Adams Ahmed, Yakubu Mohammed na Nathaniel Asamoah.
Katika Robo Fainali za awali jana, Namibia na Botswana zilifanikiwa kutinga Nusu Fainali baada ya ushindi wa matuta Jumapili Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg.
Namibia iliwatoa mabingwa watetezi Zambia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0, wakati Botswana iliwatoa wenyeji Afrika Kusini kwa penalti 7-6 baada ya sare ya bila mabao pia.
Robo Fainali ya mwisho itaendelea hivi sasa 
kati ya Msumbiji na Malawi Uwanja huo huo, Royal Bafokeng Sports Palace.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.