MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA UALIMU RUNGEMBA MUFINDI


Wahitimu  wa  kwanza wa  chuo  cha ualimu Rungemba  Mufindi
Badhi ya  wanafunzi  wanaobaki
Wanafunzi wanaobaki  wakiwaaga  wenzao kwa kwaya
Mchungaji Edga Mbadime kulia akiwa na  wachungaji  wenzake
Askafu Mkombo na Kigahe  kulia
Wageni  waalikwa wakiwa katika mahafali hayo  aliyesimama  kulia ni Mary  Mungai mkurugenzi wa shule  za Southern Highlands Mafinga
Waimbaji  wakitumbuiza katika mahafali hayo
Askofu Mulilege  Mkombo
Mmoja kati ya  wadau  aliyefanikisha kupata  kiwanja
Bw Exaud Kigahe  akihotubia katika mahafali hayo
Baadhi ya  wanahabari  wakiwa katika picha ya pamoja na mhitimu katika mahafali  hiyo kutoka kushoto ni Neema Msafiri , Flora Kamaghe na kulia ni Clement Sanga
Kamati ya mandalizi ya  mahafali  hiyo
Viogozi  mbali mbali  wakiwa katika chuo  hicho mara baada ya mahafali
  Mgeni  rasmi katika mahafali ya kwanza  ya  chuo cha ualimu  Rungemba  wilayani Mufindi mkoani Iringa Bw Exaud Kigahe kutoka  wizara  ya  viwanda na biashara makao makuu (  wa nane kutoka  kulia) akiwa fuatiwa na mkurugenzi wa chuo hicho Askofu Mulilege  Mkombo pamoja na viongozi  wengine wa  chuo  hicho serikali na  chama tawala wakati wakiwa katika  picha ya pamoja na  wahitimu hao
 ...........................................................................................................................................................
        Na FGBLOG
KATIKA  kuhakikisha watoto  wanaotoka katika familia  na uwezo  wakiwemo yatima ,kanisa la House of Prayer shield of Faith Cristian Fellowship Church (HOPS) lenye makao makuu yake mkoani Dar es Salaam  limeanzisha chuo cha ualimu kitakachotoamafunzo ya  ualimu kwa gharama nafuu kwa  wanafunzi wake kama njia ya  kutekeleza mpango wake  wa  elimu kwanza.

MKurugenzi  mkuu  wa  chuo  hicho askofu Mulilege  Mkombo aliyasema hayo jana wakati  wa mahafali ya  kwanza  ya  chuo  hicho yaliyofanyika katika  viwanja  vya  chuo cha  Ualimu Rungemba wilaya  Mufindi  mkoani Iringa .

Alisema  kuwa hatua  ya  kanisa lake  kuanzisha utaratibu  wa kujenga chuo  hicho na shule  mbai mbali za Sekondari  nchini  ni  kuisaidia  serikali katika kusaidia  familia  maskini na  yatima  kuweza  kunufaika na elimu ya gharama nafuu  kama  njia  ya kupunguza ujinga miongoni mwa jamii ya  kitanzania hasa  ile  isiyo na uwezo  wa kusoma katika shule za  sekondari na vyuo ambavyo ada yake ni  kubwa .


" Nilipewa maoni ya  kuanzisha  chuo  hicho na Mungu  na Waumini  wa kanisa na  HOPS kwa  kutambua umuhimu  wa  elimu waliweza  kujitolea michango  yao mbali mbali ya kuanzisha  ujenzi  wa  chuo   hicho na mwaka 2013 chuo  hicho  kilianzishwa kwa  kuwa na wanafunzi 8 pekee ila kwa  sasa ni  wanafunzi 43 ndio  walioweza  kuhitimu kwa mwaka wa kwanza katika  chuo hicho....Yesu Kristo alinielekeza niwahudumie watu katika Afya  na Elimu " alisema askafu Mkombo


Kuwa moja kati ya kazi  kubwa  za kanisa  hilo ni kuwafanya  watu  wote  wamjue Mungu na  kuwarudisha  vijana waliovamiwa na nguvu  za giza katika maisha yanayompendeza  Mungu , kuwaponya walioathirika na utumiaji  wa madawa ya kulevya ,kuzuia mauwaji ya kikatili na ugaidi ili  kumrudisha mwanadamu katika utu  wa haki na kweli ,kurekebisha maadili yaliyoporomoka na kuwa huduma  hizo  zinatolewa kwa watu  wote bila kujali imani  zao ,

Askofu Mkombo alisema katika  huduma za  kijami lengo la kanisa  hilo ni  kuendelea  kujenga shule  za msingi ,sekondari na vyuo pamoja na kusaidia  kuanzisha Zahanati katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Hata  hivyo  alisema  kuwa sababu  kubwa ya  kutoa elimu kwa ada  ndogo ni moja kati ya mkakati wa kanisa hilo katika kuthamini sekta ya  elimu na kuamini  kuwa elimu ndio  dira  peke ya  mtanzania huku  likiamini  kuwa uwekezaji muhimu ni katika  sekta ya  elimu  na  sio mijini pekee bali hata vijijini ambako siku zote  wamekosa fursa 


Akielezea  mkakati  wa wilaya ya  Mufindi katika  eneo hilo la chuo cha ualimu Rungemba alisema ni kuona  eneo hilo linajengwa shule ya msingi na  sekondari kwa ajili ya mazoezi kwa  wanafunzi wa  chuo   hicho ambacho kwa sasa kinatoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti ,Diploma peke japo  baadae ni kujenga majengo  zaidi kwa ajili ya kuanza  kutoa Digrii ya kwanza na ya pili na kuwa  waumini  wapo tayari  kujenga majengo hayo  ila  wanasubiri  serikali ya  kijiji  kuwaongezea eneo la ardhi  zaidi.

Pia  askofu Mkombo alisema kuwa malengo ya kanisa ni kuona kila wilaya na mkoa wa Tanzania wanajenga  shule ,chuo ,zahanati au  Hospitali  ili kila mtanzania  aweze  kupata elimu na huduma za afya kwa gharama nafuu  zaidi .

Alisema kuwa moja kati ya changamoto katika  chuo  hicho ni  wanachuo badhi  kupata  shida ya malazi  kutokana na uchache wa mabweni ,pia  nyumba  za  walimu  pia  kukosekana kwa Hospitali ama  zahanati katika kijiji  hicho  cha Rungemba .

Akizungumza katika mahafali  yao  mgeni  rasmi Bw Exaud kigahe kutoka  wizara ya viwanda  mbali ya  kupongeza  kanisa  hilo kwa kuanzisha  chuo  hicho katika  wilaya ya Mufindi bado  alisema akiwa kama mdau wa elimu katika  wilaya ya  Mufindi ataungana mkono  na jitihada za  kanisa  hilo katika kukiendeleza  chuo  hicho na kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kusaidia ujenzi  wa mabweni .

Bw  Kigahe  alisema  kuwa yeye ni mkazi wa kijiji cha Nundwe wilaya ya  Mufindi ila amesikitishwa  zaidi  katika  zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga  kura   kuona  sehemu  kubwa ya  vijana ambao  wapo chini ya miaka 40  kushindwa  kujua kusoma na kuandika katika  wilaya  hiyo ya  Mufindi na  kutaka   chuo  hicho  kuendelea  kutoa furasa  zaidi kwa wilaya  hiyo .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI