Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) yatoa ufafanuzi kuhusu Kanuni No. 13


Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa. 
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu Kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde.
Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim.
Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Ngabo Ibrahim.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu jijini leo.
Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akiwa amezungukwa na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipotoa ufafanuzi kuhusu Kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Ngabo Ibrahim.
Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu Kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Ngabo Ibrahim.
Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu Kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Ngabo Ibrahim.


MAELEZO KUHUSU KANUNI NO.13 
UTANGULIZI: 
Kanuni ya Uwianishija Mafao ya Pensheni ya 2014 ina vipengele 15 ambavyo vinalenga kuboresha mafao ya pensheni ya wanachama, kulinda na kutetea maslai ya wanachama, kuhuisha kiwango cha uchangiaji na malipo ya pensheni ya wanachama wa mifuko mbalimbali na kutengeneza mfumo madhubuti ya Kisheria katika kuwianisha viwango vinavyohusiana na mafao ya pensheni. Kipengele cha 13 kinatoa punguzo la asilimia 0.3 kwa pensheni ya kila mwezi kutoka kwenye mafao ya mwanachama aliestaafu kwa hiari yaani kati ya miaka 55 mpaka 59. Punguzo hili hukoma pale mstaafu anapofika miaka 60.
Tumekuwa tukipokea malalamiko kuhusu kanuni hiyo, lakini Tafsiri halisi ya kipengele cha 13 cha kanuni za uwianishaji wa mafao, ni kwamba mwanachama anayestaafu kwa hiari atapunguziwa asilimia 0.3 kwa mwezi sawa na asilimia 3.6 kwa mwaka hadi pale atakapofika umri wa kustaafu wa miaka 60. Hivyo si sahihi kusema kwamba kipengele hicho cha 13 cha kanuni kinakata asilimia 18  ya mafao ya  mstaafu kwa mwaka. 

Badala yake mwanachama anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 59 anakatwa asilimia 3.6 tu kwa mwaka. Mwenye miaka 58 anakatwa jumla ya asilimia 7.2 tu kwa Mwaka, Hali kadhalika mwenye miaka 57 anakatwa jumla ya asimilia 10.8 kwa mwaka. Kwa yule anayestaafu akiwa na miaka 55 atakatwa jumla ya asilimia 18 katika kipindi cha miaka mitano au miezi 60. 

Hata hivyo pamoja na punguzo la asilimia 0.3 bado mstaafu wa hiari anamzidi yule anayestaafu akiwa na miaka 60 kwa asilimia 10. Bila punguzo hilo anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 55 anamzidi mwenzake wa miaka 60 kwa asilimia 28. Hii inaondoa usawa wa mafao katika hifadhi ya Jamii. Jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na vyama vya wafanyakazi na wanachama kwa ujumla. 

HITIMISHO
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama na kutoa wito kwa wanachama na wadau wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na kwa watanzania kwa ujumla kuunga mkono Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kuboresha mafao na kuifanya sekta kuwa endelevu.  
 Mamlaka imeanza kufanyia kazi malalamiko ya wastaafu,iwapo kuna malalamiko yoyote kutokana na utekelezaji wa kanuni hii basi wanachama wasisite kuwasiliana na Mamlaka ili yapatiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo.

Mwisho tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata toka kwa vyama vya Wafanyakazi pamoja na Shirikisho lao; chama cha Waajiri; vyombo vya habari pamoja na Serikali kwa ujumla.
Ikumbukwe kuwa:
Asilimia 0.3 ni kwa pensheni ya mwezi na si kwa mkupuo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mahusiano na uhamasishaji
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P 31846,
Simu: +255 222761683/8, 
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI