Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa Serikali wa Dkt. Servacius Likwelile
akiwa pamoja na Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya wakati mara tu
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Abidjan.
Akizungumza na
vyombo vya habari mchana huu DKt.Likwelile ambaye ni amemuwakilisha Waziri wa
Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia amesema kuwa,”Mkurungezi wa Kanda
ametoa ripoti ya mwaka, ameelezea ni namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa
ukifanya kazi za maendeleo, ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika. Nchi hizo
ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda,
Kenya, Ethiophia na Visiwa vya Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri. Alisisitiza Likwelile.
Likwelile
amefanafua kuwa, “Mkurugenzi wa ukanda wanchi za Afrika ameelezea jinsi uchumi unavyokua kwa kasi kubwa kwani
umekua kwa asilimia sita mpaka saba na ukuaji huu wa uchumi unawanufaisha watu
wote wa nchi hizo.
Ni Muhimu kuwekeza
kwenye reli hii itawapunguzia wananchi usumbufu wanaoupata kwenye masuala ya
usafiri na usafirishaji wa mizigo.Aliongeza Likwelile.
Pia Likwelile
amezungumzia kuhusu kuendeleza kilimo hasa kilimo chenye tija. alisema kuwa
kilimo cha biashara humuongezea kipato mwananchi
wa chini na kumfanya kujikwamua kwenye hali ya kimasikini.
Aidha mwenyikiti
amezungumzia suala nishati hasa nishati ya umeme ili tuweze kuendelea ni muhimu
kusimamia suala la umeme kwa kikanda. Hii itapelekea nchi zote za Afrika kunufaika
na masuala ya maendeleo kiujumla kwa nchi hizo za kikanda.
“ Mwaka huu ni
mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais, Aidha ukanda wa nchi za Afrika unapenda
kumshukuru raisi aliyepita Dkt. Kaberuka kwa kazi nzuri aliyoifanya kwani
ameziacha nchi katika hali nzuri sana” Alisisitiza Likwelile
Mwisho Likwelile
alifafanua kuwa, “Benki ya Maendeleo ya Afrika imetambua umuhimu wa kazi na
mchango mkubwa alioutoa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na ndio maana imemualika
katika Mkutano huu wa mwaka kutokana na kazi zuri aliyoifanya.
Imetolewa na Msemaji wa
Wizara ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
ABIDJAN
25 MEI 2015.
Comments