MWANAHARAKATI WA BURUNDI AOMBA MKUTANO WA KESHO WA MARAISI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOMRUHUSU RAIS NKURUNZIZA KUGOMBEA MUHULA WA TATU.

             

 Mwenyekiti wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau. 
 
 Mwenyekiti wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mvutano wa kisiasa dhidi ya rais wa nchi hiyo ambapo amewataka viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaokutana leo jijini Dar es Salaam kutokubaliana na maamuzi ya Rais Pierre Nkuruzinza kuwania nafasi hiyo kwa awamu ya tatu.
Hapa mwanaharakati huyo akisisitiza jambo kwa wanahabari.
 
Salha MohamedMWENYEKITI wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau, amewataka viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kutokubaliana na maamuzi ya raisi Pierre Nkurunzinza kuwania kiti cha urais kwa awamu ya tatu.Hali hiyo itapelekea kuendelea kutoondoka barabarani hadi hapo rais huyo atakaposema hatawania kiti cha urais kwa awamu hiyo ya tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti huyo alisema wanawataka viongozi wa nchi za afrika mashariki kumshawishi raisi huyo au kumlazimisha kuachana na maamuzi hayo ya kugombea madaraka ya urais kwa awamu ya tatu.
Pia kumtaka rais huyo kutoa silaha ambazo zimezagaa kwa wananchi hao, na kuandaliwa mazingira bora ya chaguzi na utendeke kwa hali ya kuwa wanasiasa wanakuwa huru na kuacha kuwindwa na kufungwa.
Hayo yamejiri baada ya rais huyo kutangaza nia ya kuwania kiti hicho kwa awamu ya tatu ambayo ni kinyume cha sheria ya katiba ya nchi hiyo.
“Hali hii inaleta kumbukumbu ya historia ya zamani kwani yalitokea kama haya ambapo kulipelekea machafuko, na kuuawa kwa wale wote ambao hawapo sambamba na maamuzi ya rais huyo,” alisema.
Alisema hali ya usalama nchini humo ni ndogo kwani silaha zimezagaa kwa wananchi, wanajeshi na mgambo ambapo inahatarisha hata usalama wa nchi zilizopakana na nchi ya Burundi.
“Katika kipindi cha miaka kumi, hakuna hata siku moja ambayo raisi Pierre Nkuruzinza kuandaa kikao rasmi baina yake na vyama vya kisiasa na badala yake huweka wawakilishi wake, hakuna hata ndugu zake ambao wamechangia kukataa muhula huo si halali anakuwa adui yake na wengine kufukuzwa kazi na kuwindwa hadi kuuawa,” alisema.
“Huu muhula wa tatu hauna faida na taifa letu na ndiyo maana tumenzisha vuguvugu ambapo hatutaacha hadi hapo atakapo sema ameachana na awamu hiyo ya tatu, kwani amepata ushauri kutoka sehemu mbalimbali kama muungano wa watu wa ulaya, Afrika yenyewe, nchi za jumuia ya Afrika mashariki lakini pia kwa maaskofu, hivi sasa anataka kuwa sababu na chanzo cha machafuko kwasababu raia wa burundi kwa uoga wamekimbia nchi yao,” alisema.
Aidha alimpongeza rais wa Jakaya Kikwete kukubali kuwakaribisha wananchi wa Burundi na kuwapatia hifadhi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*