Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Joseph Blatter ametuma salamau za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.

Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.

Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.

Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans  na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio.

Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA