RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI WAWILI WA MAHAKAMA YA RUFAA


Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia Jumamosi iliyopita, Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, jana, Alhamisi, Aprili 30, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.

Taarifa hiyo imewataja wajaji hao kuwa ni Jaji Augustine Gherabast Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha, ambao wote wamekuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa Novemba 28, 2006.

Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara, Mahakama Kuu, Dar Es Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.

Aliajiriwa kama Hakimu Mkazi Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka 1986.

Naye Jaji Mugasha, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam. Alikuwa Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu 2009 hadi alipohamishiwa Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.

Aliajiriwa kama Wakili wa Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo huo, 1983.



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU