Vingozi wa vijana mkoa wa Iringa wakiwa katika kikao cha tathimini ya ziara ya katibu mkuu wao Taifa |
UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempatia tuzo maalum ya uongozi bora katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda baada ya kazi kubwa ya kukijenga chama aliyoifanya ndani ya wilaya za mkoa wa Iringa .
Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw ElishaMwampasha amekabidhi tuzo hiyo leo wakati wa kikao cha tathimini ya ziara yake ya siku tatu mkoani Iringa .
Alisema kuwa UVCCM Taifa imepata kuwa na makatibu wengi ila utendaji kazi na uwajibikaji wa vitendo ambao ameufanya katibu huyo Bw Mapunda ndani ya mkoa wa Iringa ni wa mfano na wao kama vijana wamependezwa na utendaji wake hivyo kulazimika kutoa tuzo hiyo kama ishara ya kumpongeza na kumtia moyo ili kuzidi kuendelea na utendaji huo .
"Mheshimiwa katibu mkuu wa UVCCM Taifa sisi vijana wa mkoa wa Iringa tumependezwa na utendaji kazi wako na wewe ni mmoja kati ya viongozi wa mfano katika Taifa letu hivyo tunaomba kukutunuku tuzo ya maalum ya heshima ya uongozi bora "
Katika hatua nyingine katibu huyo wa UVCCM mkoa wa Iringa alimpongeza Bw Mapunda kwa kuchangia shughuli mbali mbali za maendeleo katika ziara yake na kuwa agizo lake la kuwataka vijana kusaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Idodi ambalo liliungua moto wamelipokea na watafanya zaidi ya kufyatua tofari wataanza ujenzi hata kwa kuchimba msingi .
Kwa upande wake Bw Mapunda mbali ya kuwashukuru vijana hao kwa kutambua mchango wake ila alisema kazi hiyo anayoifanya ni sehemu ya majukumu yake na hakutegemea kupewa tuzo hiyo ya heshima kwani kama ni sifa ni za vijana wote nchini ambao wanatoa ushirikiano kwake .
"Sikutegemea kama mmeniandalia tuzo hii mimi kuja huku Iringa na kufanya yote niliyoyafanya ni kwa ajili ya kujenga chama chetu sote na kuwaonyesha wapinzani kuwa CCM ni kazi kwa vitendo zaidi na sio porojo za majukwaani ambazo hazina faida kwa wananchi"
Ziara ya kiongozi huyo mkoani Iringa imeonekana kuwa na matumaini mapya kwa CCM katika jimbo la Iringa mjini ambalo linaongozwa na mbunge mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae amesema kuwa muda wake wa kukabidhi jimbo CCM umefika na kuwataka CCM hasa vijana kutofanya siasa za wapinzani za maneno na badala yake kushiriki katika shughuli za maendeleo na wananchi.
Comments