Washauriwa kutumia umeme kwa shughuli za Kiuchumi

7
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akipokelewa na Wazee wa Kijiji cha Wangi na Viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake kijijini hapo.
8
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizizitiza jambo wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Wangi, Wilayani Mpwawa, Mkoani Dodoma kuhusu hatua zilizofikiwa za Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA na TANESCO.
2
Mtaalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Kanda ya Kati , Mhandisi Michael Kessy akieleza jambo kuhusu Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini. (TANESCO). Wengine wanaomsikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene na Wataalamu kutoka TANESCO.

1
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene , akishauriana jambo na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) (Kanda ya Kati) na Mtaalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lwihomelo wilayani Mpwapwa, Mkoani Ddodoma, Waziri Simbachawene alifika kijijini hapo kuwaeleza wananchi kuhusu hatua iliyofikiwa ya Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, katika eneo la kijiji hicho. Wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho na Kiongozi wa CCM wilayani hapo
3
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Kijiji cha Wota wakati akiwasili kijijini hapo kuongea na wananchi kuhusu hatua ya Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini , Awamu ya Pili kijijini hapo.
4
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa kwanza kushoto), akiwatambulisha Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambao aifuatana nao katika ziara ya kueleza utekelezaji wa Mradi huo katika kijiji cha Wota.
5
Mmoja wa wananchi katika kijiji cha Lwihomelo, Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma akiwasilisha kero ya Kijiji kwa niaba ya wanakijiji kwa Waziri wa Nishati na Madini, George simbachawene wakati wa ziara yake kijijini hapo.
6
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Wangi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipotembelea kijijini hapo wakati wa ziara yake ya kueleza hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili katika Kijiji hicho.
…………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Mpwapwa-Dodoma
Wananchi wa Vijiji mbalimbali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma vikiwemo vya Wangi na Lwihomelo, wametakiwa kutumia Umeme kwa shughuli za kiuchumi wakati vijiji hivyo vitakapounganishwa na huduma hiyo badala ya kutumia nishati hiyo kwa ajili ya mwanga tu.
Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma wakati akieleza hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuviunganisha vijiji hivyo na huduma ya Umeme unaotokana na Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
Aidha, ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa nishati ya umeme ni kichocheo kikuu cha ukuaji uchumi hivyo, amewataka wananchi hao kuitumia nishati hiyo kwa kutengeneza ajira mbalimbali zinazotokana na nishati hiyo.
“Kumbukeni kwamba Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi hii, lakini vilevile miradi hii ni uwekezaji mkubwa hivyo, tumieni umeme katika shughuli za kiuchumi zitazowezesha kuchangia gharama za uwekezaji huu mkubwa kupitia shughuli zenu.
Vilevile, katika ziara hiyo, Waziri Simbachawene amewaasa wananchi hao kuandaa mazingira ya nyumba bora zitakazokuwa na viwango vya kupokea nishati hiyo. “Andaaeni nyumba zenu na mazingira wakati mnasubiri kuunganishwa na nishati hii”, amesema Simbachawene

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA