WATANZANIA WAISHIO AFRIKA KUSINI WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI KUISAPOTI STARS LEO, LAKINI IKAWABOA!


Watanzania waishio miji mbalimbali Afrika Kusini walijitokeza kwa wingi Jumatatu usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kuishangilia timu yao ya taifa, Taifa Stars ikicheza na Swaziland katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Kombe la COSAFA mjini Rusternbug, Afrika Kusini. Bahati mbaya Taifa Stars ilifungwa 1-0.
Wa pili kushoto ni aliyewahi kuwa Meneja wa Yanga SC, Karigo Godson ambaye kwa sasa anafanya biashara Afrika Kusini
Vijana walijitahidi kuisapoti timu yao, lakini bahati haikuwa yao leo
Wake kwa waume, walichukua jezi, bendera, ngoma na vuvuzela kwenda kuishangilia timu ya nchi yao, lakini wakaondoka wanatukana wachezaji na makocha baada ya mchezo mbaya na kufungwa na timu ambayo wao wanaamini ni dhaifu
Wapo waliokuja kutoka Johannesburg na bango lenye picha ya baba wa taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere lenye ujumbe; "Wanadamu wote ni ndugu zangu na Afrika Moja

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*