Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha,
Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu
mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika
Hoteli Njuweni Kibaha. Bi.Ingiahedi alisema kuwa Serikali ya Tanzania
ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya
fedha katika ngazi zote. Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na
mafanikio yanayojitokeza na changamoto.
Alisema
kuwa Mpaka sasa mradi huo umepata mafanikio makubwa hasa ya kuweka mfumo
mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na
fedha zinatoka kwa wakati,Alibainisha kuwa bajeti ya mwananchi
inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha na kuwa mfumo wa malipo
umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha.
Baadhi ya
waandishi wa Habari wakiwa katika warsha ya siku tano kuhusu kuhusu
mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika
Hoteli ya Njuweni Kibaha.
Serikali
ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya
matumizi ya fedha katika ngazi zote. Mradi huu umekuwa wa awamu 4
kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.
Awamu ya kwanza (I) ilikuwa kutoka mwaka 1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi, kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuzana kuimarisha uchumi mpana.
Awamu ya pili (II) ilikuwa
kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na
kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma
kwa kutumia njia rahisi na nyepesi. Aidha awamu hiyo ilizingatia pia
uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya
kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.
Awamu ya tatu (III) ilikua
kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kuna
kuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katikaTaasisi mbalimbali za
kifedha.
Awamu ya nne (IV) ya
mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1
Julai, 2012. Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika
kuonge za nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya mwaka 2025, hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa
miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016 na MKUKUTA
(MkakatiwaKukuzauchumi Tanzania)/ MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi
Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchum
Comments