YANGA YAMNASA BEKI KISIKI WA KMKM, YAMSAJILI KIPA KINDA WA KAGERA SUGAR

HAJI MWINYI AKISAINI MKATABA KUICHEZEA YANGA, LEO MBELE YA MENEJA WA YANGA, HAFIDH SALEH.

Yanga imefanikiwa kumsajili beki Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar.

Haji Mwinyi amesaini kuichezea Yanga leo na sasa yuko njiani kurejea kwa Zanzibar.
“Kweli Haji amesaini Yanga leo, ataichezea kwa miaka miwili na kila kitu kimeisha.
“Tuko njiani tunarejea Zanzibar, shughuli zote zimefanyika kwenye makao makuu ya Yanga,” kilieleza chanzo.
Mwinyi alikuwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano ya Kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini.
Pamoja na Mwinyi, Yanga imefanikiwa kumnasa kipa wa Kagera Sugar, Benedicto Tinocco.

Tinocco licha ya kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana, pia aliwahi kuwa kipa bora wa michuano ya Copa Coca Cola

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI