YANGA YATANGAZA KUMFUNGULIA MASHITAKA ALIYETANGAZA UCHAGUZI KINYEMELA


‘Uswahili’ wamponza Kaswahili, Yanga yafungua kesi mahakamani, TFF
Uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza kumfungulia mashtaka mahakamani na kumfikisha katika kamati ya nidhamu ya TFF, mdau wa soka Bw Fransic Kaswahili kwa kitendo cha kutangaza kwenye vyombo vya habari uwepo wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, jamboa ambalo uongozi umekanusha.

Mei 14, 2015 Kaswahili ambaye alijitambulisha kama katibu wa kamati ya uchaguzi wa Yanga, alisambaza taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa kutakuwa na uchaguzi mkuu ambao utafanyika July 12, mwaka huu huku fomu za kugombea zitaanza kutolewa Mei 17, mwaka huu katika makao makuu ya klabu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Yanga, Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kupuuzia tangazo la ndg Kaswahili na kwamba wameamua kumfikisha kwenye kamati ya maadili ya TFF kwani wameona kumvua uanachama haitatosha, hivyo wamemua kuanzia kwa TFF.

Aidha, wameamua kumfungulia mashtaka ya jinai na madai makosa yafuatayo:
i)                      Taarifa yake ilikuwa ni uchochezi wa kuvuruga amani ndani ya klabu hiyo kwa kuitisha uchaguzi batili, akiwa si kiongozi wa Yanga.
ii)                   Kuidhalilisha klabukwa kutumia jina lake na kujiita katibu wa kamati ya uchaguzi wakati akijua fika si kiongozi wa kamati yoyote na mbaya zaidi si mwanachama hai kwa kile alichoeleza Dk Toboroha kuwa hajalipia kadi ya uanachama tangu 2012, hivyo kitendo cha kutolipia kadi yake baada ya ya miezi sita, kisheria unakuwa si mwanachama hai, hivyo hata uchaguzi ungekuwepo, bado asingeruhusiwa kupiga kura mpaka achukue kadi mpya kwa wazabuni wao; CRDB na Posta Bank.
iii)                 Kuzungumzia masuala ya klabu bila kuwasiliana na sekritariet husika
iv)                 Ilikuwa ni njia ya kuwatapeli wanachama wa Yanga kwa kutangaza bei za fomu za uchaguzi huo BATILI.

Hata hivyo Kasawahili alikuwa amepewa nafasi ya kukanusha taarifa zake kupitia ‘media’ alizowapa taarifa hiyo kufikia leo 6:00 mchana, lakini akashindwa, hivyo suala lake linatua TFF na mahakamani. Mkutano wa waandishi ulifanyika saa 7:00 ili usubiri taarifa yake ya kukanusha.
  
DK Tiboroha amefafanua kuhusu Kaswahili aliwahi kuwa katibu wa kamati ya uchaguzi katika utawala uliopita kabla ya kamati hiyo kuvunjwa mwaka jana mwezi Machi, kwa ajili ya kupisha uchaguzi mkuu mwingine ambao ulikuwa ufanyike mwaka jana, lakini kwa ridhaa ya wanachama wakauongozea muda uongozi wa Manji kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Alex Mgongolwa muda wowote atatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu.
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi utawala uliopita, Mh. Jaji Mkwawa amejitoa katika timbwili la Kaswahili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA