Zuma ataka uchaguzi kuahirishwa Burundi

Rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma amekuwa
kiongozi wa hivi karibuni anayetaka uchaguzi wa urais nchini Burundi kuahirishwa.
Akizungumza baada ya mkutano wa kieneo nchini Angola,Bwana Zuma alisema kuwa uchaguzi huo haupaswi kufanyika hadi hali ya amani itakaporudi nchini humo.
Maandamano yanaendelea katika mji wa Bujumbura kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliopita.
Rais wa taifa hilo amekana madai ya kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watekelezaji wa shambulio hilo.
Wafanyikazi wa mahospitali nchini Burundi awali walielezea kuwa kumekuwa na mshambulizi ya kulipiza kisasi ambapo polisi wamekuwa wakiwajeruhi wanajeshi waliodaiwa kuhusika na jaribio hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI