AZAM YAZIBWAGA SIMBA, YANGA KWA UBORA WA KLABU AFRIKA

                          


AZAM FC imezibwaga klabu kongwe nchini Simba na Yanga kwa ubora wa klabu barani Afrika katika orodha iliyotolewa na mtandao wa FootballDatabase.
Katika orodha hiyo inayofungwa na Indeni FC ya Zambia iliyoshika mkia kwenye nafasi ya 431 ya klabu zenye sifa ya kushindanishwa kwa ubora Afrika, Azam FC ndiyo inaoongoza Tanzania ikiwa nafasi ya 324 barani.
Simba inakamata nafasi ya pili nchini ikiwa nafasi ya 332 barani Afrika wakati Yanga haimo hata kwenye orodha kutokana na kukosa sifa za kushindanishwa.
5 BORA
Mabingwa wa Afrika, klabu ya TP Mazembe ya DRC wanakocheza Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu inaongoza bara la Afrika ikifuatwa na El-Marreikh (Sudan), Vita Club (Congo), Al-Hilal Omdurman (Sudan) na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inayokamilisha tano bora barani.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia FC wameunga na Yanga kukosa sifa ya kuwamo katika orodha ya klabu hizo 431 zinazostahili kushindanishwa kwa ubora wa soka.
Klabu ya Zesco United ya Zambia anayoichezea mshambuliaji Mtanzania Juma Luizio, imefanya vizuri katika ubora huo na kukamata nafasi ya 133.
Kuzijua klabu zote 431 zilizotinga katika orodha hii, ingia kwenye mtandao wa FootballDatabase.(VICTOR)
1. TP Mazembe – DRC
2. Al-Merreikh – Sudan
3. AS Vita – DRC
4. Raja Casablanca – Morocco
5. Al Hilal Omdurman – Sudan
6. Kaizer Chiefs – South Africa
7. Esperance – Tunisia
8. Cotonsport – Cameroon
9. Etoile du Sahel – Tunisia
10. Dynamos – Zimbabwe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*