AIBU YETU WENYEWE, MABINTI WAPIGWA 4-0 NA ZAMBIA CHAMAZI

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeanza vibaya mbio za kuwania tiketi ya fainali za Afrika, baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 4-0 na Zambia Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ilikuwa huzuni kwa Watanzania wote waliojitokeza Uwanja wa Azam, Chamazi wakiongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi namna ambavyo Tanzanites walivyonyanyaswa na mabinti wenzao shupavu wa Zambia.
Tanzanites inayofundishwa na mzalendo, Rogasian Kaijage leo ilizidiwa kabisa na Shepolopolo Uwanja wa Azam na kujikuta hadi mapumziko ikiwa tayari imekwishabugizwa 3-0.
Barbara Banda wa Zambia akishangilia baada ya kufunga bao la tatu Chamazi leo
Irene Lungu wa Zambia (kushoto) akimtoka Maimuna Hamisi wa Tanzania
Shelider Boniphace wa Tanzania kulia akipambana na Lwendo Chisamu

Mabao ya Shepolopolo yalifungwa na Memory Phiri dakika ya nne, Irene Lungu dakika ya 20 na Barbara Banda dakika ya 33.
Kipindi cha pili, Zambia walirudi na moto wao tena na kufanikiwa kupata bao la nne, mapema tu dakika ya 50 kwa penalti kupitia kwa Marry Wilombe.
Refa Batouli Ibrahim wa Sudan alitoa penalti hiyo baada ya Anastazia Anthony kumfanyia faulo mshambuliaj wa Zambia, Memory Phiri.
Sasa Shepolopolo inatakiwa kwenda kushinda mabao 5-0 ugenini ili kusonga mbele.
Kikosi cha Tanzania; Najjiat Abbas, Zuwena Aziz, Happiness Hezron, Maimuna Hamisi, Anastazia Anthony, Donisia Daniel, Hamisa Athumani, Neema Paulo, Asha Shaaban Hamza/Janet Cloudy dk40, Shelider Boniphace na Stumai Abdallah. 
Zambia; Hezel Natasha Nali, Mary Wilombe/Osala Kaelo dk75, Margaret Belemu, Martha Tembo, Mlika Limwanya, Lwendo Chisamu, Esther Mukwasa, Irene Lungu, Grace Chanda, Barbara Banda na Memory Phiri/Agnes Musesa dk83. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.