JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya simu “ mkuupolisi”
Ofisi ya Inspekta
Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax na. (022) 2135556
S.l.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: Dar es Salaam.
16/07/ 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunaelekekea kipindi
hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr na ambapo wananchi wenye imani ya
kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na
muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe, Jeshi la Polisi
nchini linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo
kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa
amani.
Jeshi la Polisi nchini
linapenda kuwaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi
wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye
maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine
yote.
Aidha, tahadhali zichukuliwe kwa wale wote ambao
watakuwa wakitumia barabara ikiwemo maderera na watembea kwa miguu, kuwa makini
kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na
pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Jeshi la Polisi
linaendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa haraka kwenye vyombo vya dola
juu ya kitu chochote ama mienendo ya watu watakaowatilia shaka mahali popote
kwani taarifa hizo za haraka zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.
Vilevile
wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi
ama bila mtu na endapo italazimika basi ni vema watoe taarifa kwa majirani zao
kwa ajili ya usalama.
TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID
–EL-FITR
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
Comments