JK APATA TUZO YA UTAWALA BORA AFRIKA!

RAIS Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo na Taasisi ya African Achievers Awards, yenye makao makuu Afrika Kusini, kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha, kuendeleza na kudumisha Utawala Bora, kwa miaka 10 ya uongozi wake.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ilisema Kikwete anaungana na watu wengine wachache waliowahi kupokea tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa na kutolewa kwa mara ya kwanza kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana la Afrika Kusini, Desmond Tutu, mwaka 2011.
Askofu Tutu alipewa tuzo kufuatia mapambano yake kutetea haki za binadamu, usawa na amani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa watu zaidi ya 1,202, ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye Jopo la Kimataifa linalojitegemea,lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini, waliokaa na kufanya uteuzi.(P.T)
Ilisema, kutokana na tunuku hiyo, Rais Kikwete alialikwa Afrika Kusini kupokea tuzo hiyo, kwenye sherehe iliyofanyika jana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Sandton, mjini Johannesburg.
Hata hivyo, kutokana na kukabiliwa na shughuli nyingi nyumbani, Rais Kikwete amewakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Asha-Rose Migiro, kwenye sherehe ya kupokea tuzo hiyo, ambako pia atatoa mada kuhusu “Umoja wa Afrika: Fursa na Changamoto (Africa’s Unity: Prospects and Challenges) “ kwa niaba ya Rais Kikwete.
Tuzo za African Archievers Awards zinalenga kuwatambua watu binafsi na taasisi ambazo zimejitambulisha kwa michango yao kwa ustawi na maendeleo ya Bara la Afrika.
Mtendaji wa African Achievers Awards, Rex Indaminabo katika barua ya kumjulisha Rais Kikwete kuhusu uteuzi huo alisema, “ Uongozi wa African Achievers Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea tuzo ya 2015 African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora Barani Afrika".
"...Ni kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi ya Uongozi na Menejimenti wanakuandikia kukupongeza kwa kuteuliwa kwenye orodha ya mwisho na hatimaye kuwa mshindi wa Tuzo ya African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora katika Afrika.”

Tuma Maoni

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*