UONGOZI wa chama cha mapinduzi (CCM), wilaya ya Monduli umekanusha taarifa ya madai ya waliokuwa madiwani wake kukimbilia Chadema kwa kile kilichoelezwa kukasirishwa kwa hatua ya CCM kutompitisha mbunge wa jimbo hilo Edward Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha Urais.
Kwa mujibu wa katibu wa CCM wilaya hiyo Elifas Kimaro ni madiwani watatu tu ndio walioasi chama hicho na sio wote kama ilivyoelezwa hapo awali na mmpja wa madiwani waliohamia.chadema pamoja na viongozi wa.chama hicho.
Kimaro alisema waliokuwa madiwani wa CCM katika wilaya.hiyo wamechukua fomu za kuwania kwa mara nyingine nafasi zao katika uchaguzi ujao.
Aliwataja madiwani walioasi katika chama hicho ni pamoja na Julius Kalanga diwani wa Lepurko aliyejipambanua kama kiongozi wa madiwani wenzake waliohamia chadema, Edward Lenanu diwani wa Meserani na .....
Kimaro alisema chama cha chadema kinataka kujichukulia umaarufu wilayani humo lakini.uongozi wa ccm umejipanga.kuhakikisha unaendelea kuongoza wilaya.hiyo na kwamba tayari wana uhakika wa kuchukua kata zote ikiwemo za madiwani waliokiasi chama hicho na kukimbilia upinzani.
Comments